Mhandisi Gilliard Luyoka akizungumza kwa niaba ya Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda Magharibi-Mpanda wakati wa mafunzo hayo.
Mwenyekiti wa KATAREMA, William Mbogo (kulia) akiuliza swali kwa Mtaalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Idd Mganga (kushoto), akimsiliza kwa ajili ya kumpatia jibu.
Baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini wakifuatilia mafunzo hayo.
Mtaalamu
kutoka Wizara ya Nishati na Madini Kitengo cha Leseni, Idd Mganga akiwasilisha
mada wakati wa mafunzo hayo.
Na Mohamed Seif, Nishati na Madini
HATIMAYE mafunzo ya matumizi ya mfumo wa huduma ya leseni kwa njia ya mtandao yaani Online Mining Cadastre Transactional Portal
(OMCTP) kwa wachimbaji madini mkoani Katavi yamemalizika.
Mafunzo
hayo ya siku moja yamefanyikia kwenye ukumbi wa mikutano wa Idara ya Maji,
mjini Mpanda na kuhudhuriwa na wachimbaji wadogo wa madini kutoka maeneo
mbalimbali ya mkoa huo yakiwa yamelenga kuwapatia uwezo wachimbaji madini wa
kuutumia mfumo huo.
Akizungumza
kwa niaba ya Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda Magharibi-Mpanda, Mhandisi
Gilliard Luyoka aliwakumbusha wachimbaji hao kuhakikisha wanafika kwenye Ofisi
ya madini ili kusajiliwa kwa ajili ya kutumia mfumo huo.
Pamoja na malengo mengine, inaelezwa kwamba Mfumo
huo umeanzishwa ili kutekeleza agizo la Serikali la kutaka Wizara na taasisi za
Serikali ziwe zinapokea malipo ya Serikali kwa njia za kielektroniki.
Mfumo wa
Huduma za Leseni kwa njia ya mtandao ulizinduliwa rasmi mnamo tarehe 8 Juni,
2015.

No comments:
Post a Comment