Rais Abdel Fattah al-Sisi wa Misri, ameidhinisha hatua mpya za kupambana na ugaidi, ambazo zimezua utata zenye nia ya kuimarisha uwezo wa taifa hilo kukabiliana na maasi ya waislamu wenye itikadi kali.
Wale watakaopatikana na hatia ya kubuni au kuongoza makundi ya kigaidi, watakabiliwa na adhabu ya kifo au kifungo cha miaka kumi au maisha jela.
Nao waandishi habari ambao watapingana na ushahidi dhidi ya wanamgambo wanaoshambulia taifa hilo, watapigwa faini ya hadi dola elfu 25.
Makundi ya kutetea haki za kibinadamu yamesema kuwa rais Abdel Fattah al-Sisi, atatumia sheria hizo mpya kuwafungia wapinzani wake na pia kuwazima waasi au kupinga uhuru wa kujieleza. Mamia ya walinda usalama wameuwawa katika mashambulizi ya wanamgambo hasa katika maeneo ya rasi ya Sinai.
Kundi ambao linatekeleza uhalifu mkubwa Nchini humo limetangaza bayana kuunga mkono jitihada za wanamgambo wa Islamic State.
No comments:
Post a Comment