TANGAZO


Monday, July 27, 2015

Ukawa wamkaribisha Lowassa kwenye Vyama vyao

*Aanza kujadiliana na viongozi wa Chadema jijini Dar
Mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), James Mbatia wa NCCR-Mageuzi, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akitoa taarifa ya umoja huo, kuhusu kumkaribisha Ukawa aliyekuwa mtangaza nia wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), aliyekatwa katika hatua za awali, Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa katika moja ya vyama vya umoja huo. Wengine ni Wenyeviti wenza wa umoja huo, Profesa Ibrahim Lipumba (katikati) wa Chama cha Wananchi (CUF) na Freeman Mbowe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.blogspot.com)
Mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Profesa Ibrahim Lipumba (wa pili kushoto) wa Chama cha Wananchi (CUF), akijibu maswali ya waandishi wa habari, wakati wa mkutano huo, jijini leo. Wengine ni wenyeviti wenza wa umoja huo, Freeman Mbowe (kushoto) wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), James Mbatia (wa pili kulia) wa NCCR-Mageuzi na Emmanuel Makaidi (kulia) wa National League for Democracy (NLD).
Mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), James Mbatia wa NCCR-Mageuzi, akijibu maswali ya waandishi wa habari, Dar es Salaam leo. Wengine ni Wenyeviti wenza wa umoja huo, Profesa Ibrahim Lipumba (katikati) wa Chama cha Wananchi (CUF) na Freeman Mbowe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). 
Wenyekiti wenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Profesa Ibrahim Lipumba (kushoto) wa Chama cha Wananchi (CUF), James Mbatia (kulia) wa NCCR-Mageuzi na Freeman Mbowe (katikati) wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakitakiana heri baada ya mkutano huo.
Wenyeviti wenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kutoka kushoto, Profesa Ibrahim Lipumba wa Chama cha Wananchi (CUF), Freeman Mbowe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), James Mbatia wa NCCR-Mageuzi na Emmanuel Makaidi wa National League for Democracy (NLD), wakiwa wameshikana mikono kuonesha umoja wao baada ya kuzungumza na waandishi wa habari, Ofisi Kuu ya CUF, Buguruni Dar es Salaam leo, kutangaza kumkaribisha Ukawa aliyekuwa mtangaza nia wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), aliyekatwa katika hatua za awali, Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa. 
Wenyeviti wenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kutoka kushoto, Profesa Ibrahim Lipumba wa Chama cha Wananchi (CUF), Freeman Mbowe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), James Mbatia wa NCCR-Mageuzi na Emmanuel Makaidi wa National League for Democracy (NLD), wakifurahia jambo mara baada ya mkutano huo na waandishi wa habari, Ofisi Kuu ya CUF, Buguruni Dar es Salaam leo.
Waziri Mkuu mstaafu, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa (kushoto mwenye suti nyeusi), akiwa katika kikao cha mazungumza na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakati wakijadili yeye kujiunga na chama hicho pia kupewa ridhaa ya kuwania nafasi ya Urais wa Tanzania kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa). (Na Mpigapicha wetu) 
Waziri Mkuu mstaafu, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa (mwenye suti nyeusi), akizungumza na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakati wa kikao cha siri kilichofanyika katika moja ya Hoteli jijini Dar es Salaam leo. Kikao hicho kinasemekana kilijadili yeye kujiunga na chama hicho pia kupewa ridhaa ya kuwania nafasi ya Urais wa Tanzania kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa). Kushoto ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Wilbrod Slaa, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Mwesiga Baregu na Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Peter Msigwa. (Na Mpigapicha wetu).

No comments:

Post a Comment