TANGAZO


Monday, July 27, 2015

Matamasha ya Night of Worship, Family Worship kufanyika Upanga City Christian Centre (CCC) jijini Dar es Salaam

*Semina ya Mafunzo ya Muziki na upigaji vyombo vya muziki kutolewa
Mchungaji Sam Mwangati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu matamasha ya Night of Worship na Family Worship, ambalo litatumbuzwa na kundi la muziki wa Injili la Krystaal kutoka Canada. Katikati ni Kiongozi wa kundi hilo, Mchungaji Fabian Lwamba na mpiga kinanda Michael Lwamba. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Baadhi ya wanakundi hilo, wanandugu, Kiongozi wa kundi, Fabian Lwamba (kulia), Michael Lwamba (katikati) na mpiga gitaa la bass na mwimbaji, Minister Aliston Lwamba (kushoto), wakiimba moja ya nyimbo ya kundi hilo, iitwayo, King of Glory.

KANISA la Upanga City Christian Centre (CCC)  Dar es Salaam mkabala na tawi la Chuo cha Mzumbe jijini Dar es Salaam, inawaletea semina ya mafunzo ya Muziki na upigaji vyombo pamoja na matamasha mawili ya kusisimua 'Night of Worship na Family Worship'.

Semina ya mafunzo ya muziki na vifaa vya muziki itafanyika katika ukumbi wakanisa la Upanga  CCC, kesho Julai 28 na 29, 2015 kuanzia  3:00 asubuhi hadi 9:00 mchana bure bila malipo.

Semina hii itafundishwa na wanamuziki wa nyimbo za injili kutoka Canada wanajulikana kwa jina la Krystaal.

Pia kutakuwa na tamasha la Night of Worship sikuya 31/07/2015 kuanzia saa 3:00 usiku katika ukumbi wa kanisani Upanga  CCC.

Pastor  SamMwangati, Mwenyekiti wa kundi la Next Level alisema kuwa ibada ya kumsifu na kuabudu watashirikiana na kundi la Krystaal kwa kiingilio cha shilling elfu 5,000 tu.

Pia 2/08/2015 kutakuwa na tamasha la Live Recording kuanzia saa 9 alasirihadi  12 jioni kwa kiingilio cha shilling elfu 10,000 kawaida.
VitivyaVIP kwa shilingi  30,000, viti maalum VIP plus 50,000. 

Karibuni wote kuabudu, kufurahi na familia zetu na kumsifu  Bwana.
………………………..
Pastor Sam Mwangati
Mwenyekiti wa Next Level Team

No comments:

Post a Comment