TANGAZO


Monday, July 27, 2015

Rais Jakaya Kikwete alivyowaongoza Watanzania Kuadhimisha Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa jijini Dar es Salaam

Brass Bendi ya Jeshi ikiingia kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja kuanza Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa, jijini Dar es Salaam juzi.  
Vikosi vya Jeshi vikiwa vimesimama kwa ukakamavu wakati wa maadhimisho hayo, viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam juzi. 
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa (JWTZ) , Luteni Jenerali Samweli Ndomba akisalimiana na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli baada ya kuwasili viwanja vya mnazi mmoja.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho akiwasili. 
Spika wa Bunge la Jamhuri Anne Makinda akiwasili. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Iddi. 
Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri, Dkt. Mohamed Gharib Bilal akiwasili. 
Rais Jakaya Kikwete akiwasili viwanjani. 
Rais Jakaya Kikwete akiwaongoza viongozi mbalimbali na wananchi kuimba wimbo wa Taifa. 
Rais Jakaya Kikwete, akiweka mkuki na ngao kwenye mnara wa Uhuru. 
Mkuu wa Majeshi  Jenerali Davis Mwamunyange akirejea kwenye sehemu yake baada ya kuweka sime kwenye mnara. 
Kiongozi wa Mabalozi akiweka shada la amaua. 
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Dkt. Didas Masaburi akiwa ameweka upinde na mshale kwenye mnara. 
Mwenyekiti wa Tanzania Legion akiweka shoka kwenye mnara. 
Baadhi ya wazee walioipigania Tanzania, viongozi wa dini na wageni waalikwa waliohudhuria. 
Baadhi ya wazee walioipigania Tanzania, viongozi wa dini na wageni waalikwa waliohudhuria. 
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam sheikh Alhad Musa Salum akisoma dua. 
Mchungaji Theophil Bolampete wa Kanisa Katoliki akiomba. 
Mchungaji John Komoyo, akiomba. 
Rais Jakaya Kikwete akiongoza viongozi mbalimbali kuimba wimbo wa Taifa baada ya Maadhimisho kukamilika. 
Rais Jakaya Kikwete, akiwaaga baadhi ya Mashujaa na waliopigana vita kuikomboa Tanzania. 
Rais Jakaya Kikwete, akiwaaga baadhi ya Mashujaa waliopigana vita kuikomboa Tanzania. 
Makamu wa Rais Dkt. Bilal, akiwaaga mashujaa na kisha kuondoka kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Iddi akiwaaga mashujaa na kisha kuondoka kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja. 
Spika wa Bunge, Anne Makinda, akiwaaga mashujaa na kisha kuondoka kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja.  
Baadhi ya askari wa JWTZ waliopigana vita ya kuikomboa Tanzania. 
Baadhi ya wananchi waliofika nje ya viwanja vya Mnazi Mmoja kushuhudia Maadhimisho. (Picha zote na Hussein Makame-MAELEZO)

No comments:

Post a Comment