TANGAZO


Thursday, July 16, 2015

Hospitali za Rufaa za Wilaya ya Temeke, Kinondoni na Ilala zanufaika na mashine za kuwasaidia watoto njiti kutoka Vodacom Foundation

Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation Tanzania, Renatus Rwehikiza (kushoto), akimkabidhi moja ya mashine ndogo kati ya tatu za kufyonza uchafu kwa watoto Njiti kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Magembe kwa niaba ya Hospitali tatu za rufaa za Wilaya ya Temeke, Kinondoni na Ilala. Msaada huo ulitolewa na Taasisi ya Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Pamoja na Vodacom kwa kushirikiana na Doris Mollel Foundation. Wanaoshuhudia wapili toka kushoto ni Dkt. Vicent Mboya na Doris Mollel. 
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Magembe (wapili toka kulia) akipokea Mashine ya kusaidia kupumua kwa watoto wanaozaliwa Njiti kwa niaba ya Hospitali tatu za rufaa za Wilaya ya Temeke, Kinondoni na Ilala toka kwa Mkuu wa kitemngo cha Vodacom Foundation Tanzania Renatus Rwehikiza (kulia) Msaada huo ulitolewa na Taasisi ya Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Pamoja na Vodacom kwa kushirikiana na Doris Mollel Foundation. Wanaoshuhudia wapili toka kushoto ni Dkt.Vicent Mboya, Afisa Muuguzi wa watoto wachanga Mary Machemba na Doris Mollel. 
Ofisa Muuguzi wa watoto wachanga Mary Machemba akiwafafanulia waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi mashine ya kufyonza uchafu kwa watoto wanaozaliwa Njiti inavyofanya kazi. Msaada huo ulitolewa na Taasisi ya Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Pamoja na Vodacom kwa kushirikiana na Doris Mollel Foundation. Wanaoshuhudia katika picha kutoka kushoto ni Renatu Rwehikiza, Dkt. Vicent Mboya, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Magembe na Doris Mollel. 
Daktari Kiongozi wa Hospitali ya Amana Dkt. Vicent Mboya, akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa vifaa vya ajili ya watoto wanaozaliwa Njiti katika hospitali tatu za rufaa za Wilaya ya Temeke, Kinondoni na Ilala. Vifaa hivyo vilitolewa msaada na Taasisi ya Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Pamoja na Vodacom kwa kushirikiana na Doris Mollel Foundation. 
Ofisa Muuguzi wa watoto wachanga Mary Machemba akiwafafanulia waandishi wa habari (hawapo pichani), jinsi kifaa maalumu cha mashine ya kufyonza uchafu kwa watoto wanaozaliwa Njiti kinavyofanya kazi. Msaada huo ulitolewa na Taasisi ya Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Pamoja na Vodacom kwa kushirikiana na Doris Mollel Foundation.Wanaoshuhudia katika picha kutoka kushoto ni Renatu Rwehikiza, Dkt.Vicent Mboya, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Magembe na Doris Mollel. 
Mkuu wa Vodacom Foundation Renatu Rwehikiza (kushoto), Dkt. Kiongozi wa Hospitali ya Amana Vicent Mboya, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Magembe na Doris Mollel wakimshuhudia Ofisa Muuguzi wa watoto wachanga wa Hospitali ya Amana Mary Machemba akifafanulia jinsi mashine ya kufyonza uchafu kwa watoto wanaozaliwa Njiti inavyofanya kazi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), Msaada wa kifaa hicho ulitolewa na Taasisi ya Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Pamoja na Vodacom kwa kushirikiana na Doris Mollel Foundation 
Mkuu wa Vodacom Foundation Renatu Rwehikiza, akiwaangalia watoto wachanga waliozaliwa Njiti katika hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam, alipofika hospitalini hapo kutoa msaada wa mashine maalumu za kuwasaidia watoto hao uliotolewa na Taasisi ya Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Pamoja na Vodacom kwa kushirikiana na Doris Mollel Foundation. 
Meneja biashara wa Idara ya Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Grace Lyon akiwakabidhi Vitenge wakina mama waliojifungua watoto wachanga katika hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam, walipofika hospitalini hapo kutoa msaada wa mashine maalumu za kuwasaidia watoto hao uliotolewa na Taasisi ya Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Pamoja na Vodacom kwa kushirikiana na Doris Mollel Foundation. 
Baadhi ya wauguzi wa hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam wakiwa katika ukumbi wa mkutano wakati wa hafla fupi ya kupokea msaada wa mashine mbalimbali za kuwasaidia watoto wachanga wanaozaliwa Njiti uliotolewa na Taasisi ya Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Pamoja na Vodacom kwa kushirikiana na Doris Mollel Foundation.

No comments:

Post a Comment