Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha Tridea wakiendelea na kazi.
Naibu Waziri Dkt. Kebwe akikagua baadhi ya vifungashio vya kuhifadhia vipodozi kwenye kiwanda hicho.
Naibu Waziri Dkt. Kebwe akipata maelezo kwenye chumba ya uhakiki na ubora wa vinywaji wa kiwanda cha TBL. Kulia ni Meneja Ubora wa kiwanda hicho Bi. Conchesta Ngaiza.
Naibu Waziri Dkt. Kebwe akiangalia baadhi ya mitambo ya uzalishaji bia (haionekani pichani) kwenye kiwanda cha bia chaTBL jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri Dkt. Kebwe akipata maelezo ya kuhusu baadhi ya mitambo ya uzalishaji wa bia. Kulia ni Meneja Uzalishaji wa tawi la Dar es Salaam, Bw. Calvin Martin.
Naibu Waziri akiwa kwenye picha ya pamoja ya watumishi toka Wizara ya Afya, Mamlaka ya Chakula na Dawa pamoja na Kiwanda cha Bia cha TBL.
Mtaalamu wa Maabara wa kiwanda cha Unga wa ngano cha Baharesa (Azam), akionesha wanavyohakiki ubora wa bidhaa zao.
Na Catherine Sungura, MoHSW
NAIBU Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Kebwe Kebwe amefanya ziara ya kujionea jinsi viwanda vya dawa, chakula na vipodozi vinavyofanya kazi, Mitambo pamoja na mifuko ya utekelezaji bidhaa kwa mkoa wa dar es salaam.
Dkt. Kebwe alisema ziara ameamua kufanya ziara hiyo licha ya kujionea mifumo ya utendaji kazi Ila kuweza kuvisaidia viwanda vya ndani viweze kushindana kibiashara,kuajiri watanzania wengi na kuongeza uzalishaji na pato la taifa pia.
Aidha, Dkt. Kebwe aliiagiza mamlaka ya chakula, dawa na vipodozi (TFDA), kuangalia uwezekano wa kupunguza siku ya kutathimini na kusajili dawa zinazotengenezwa na viwanda vya ndani.
"nimetoa maelekezo kwa tfda kuweza kuangalia siku za kutathimini na kusajili dawa, hii itamsaidia kusajili dawa za viwanda vya ndani haraka na kuwawezesha kutengeneza dawa nyingi zaidi na kuongeza mtaji wa kibiashara".
Hata hivyo Naibu Waziri aliitaka TFDA kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye viwanda vyote nchi ili kuweza kuhakiki wa utengenezaji bora wa dawa,vipodozi na chakula pamoja na kufahamu mapungufu na kuchukua hatua mapema ikiwa viwanda nchini havitimizi masharti ya utengenezaji bora wa bidhaa.
Naye mkurugenzi wa tfda hiiti silo amesema mamlaka yake itahakikisha na kusimamia utekelezaji wa maelekezo yote yaliyotolewa ili kukuza viwanda na kuviwezesha kufikia viwango bora vya utengenezaji wa bidhaa zinazodhibitiwa nchini.
Naibu Waziri huyo alitembelea viwanda vya Shelys Pharmaceuticals limited, Keko pharmaceutical industries (1997) limited, Tridea cosmetics limited, Tanzania Breweries limited na Bhaharesa Food Industries limited vyote vya jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment