*Ni mjasiriamali na mkazi wa Mtwara
*Wateja watakiwa kutuma neno JAY kwenda 15544
Mshindi wa kitita cha shilingi milioni 100/- kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Hamisi Khalid (kushoto) mkazi wa Mtwara akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhiwa hundi yake na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (kulia) baada ya kuibuka mshindi wa kitita hicho kupitia promosheni hiyo hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya kampuni hiyo Mlimani City jijini Dar es Salaam. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.
Mshindi wa kitita cha shilingi milioni 100/- kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Hamisi Khalid (kushoto) mkazi wa Mtwara akikabidhiwa hundi yake na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia wakati wa hafla ya kukabidhiwa hundi hiyo baada ya kuibuka mshindi wa kitita hicho kupitia promosheni hiyo. Hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya kampuni hiyo mlimani city jijini Dar es Salaam. Mlimani City jijini Dar es Salaam. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.
Rosalynn Mworia ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania (kulia) akimpongeza kwa kumpigia makofi mshindi wa kitita cha shilingi milioni 100/- kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na kampuni hiyo, Hamisi Khalid (aliyeshikilia hundi) mkazi wa Mtwara wakati wa hafla ya kukabidhiwa hundi hiyo baada ya kuibuka mshindi wa kitita hicho kupitia promosheni hiyo. Hafla hiyo ilifanyika Makao makuu ya kampuni hiyo Mlimani City jijini Dar es Salaam. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (kulia) akisoma tarakimu kwenye hundi yenye thamani ya shilingi milioni 100/- wakati wa hafla ya kumkabidhi hundi hiyo mshindi wa kitita cha shilingi milioni 100/- kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Hamisi Khalid (aliyeshikilia hundi) baada ya kuibuka mshindi wa kitita hicho kupitia promosheni hiyo. Hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya kampuni hiyo Mlimani City jijini Dar es Salaam. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.
Na Mwandishi wetu
MSHINDI wa mwingine wa milioni 100/- katika promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Hamis Khalidi (30) mkazi wa mkoani Mtwara na mjasiriamali anayeuza vifaa vya saluni za kike leo amekabidhiwa fedha zake katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam ambako amefungua akaunti.
Promosheni ya JayMillions inayoendelea ikiwa inakaribia kufikia mwisho mnamo Aprili 23, 2015 imekwishawawezesha baadhi ya wateja wa Vodacom kuwa mamilionea kwa kuweza kujinasua katika hali duni ya maisha na maisha kuwa murua na hadi kufikia sasa wamekwishapatikana washindi wawili wa milioni 100/-, washindi wanne wa milioni 10/- na washindi 39 wa milioni 1/-. Maelfu ya wateja pia wamejishindia muda wa maongezi.
Washindi wa milioni 100/- ni Uwezo Madegenge kutoka wilayani Kilolo mkoani Iringa na Hamis Khalidi ambaye amekabidhiwa kitita alichojishindia. Washindi wa milioni 10/- ni Zuena Rajabu mkazi wa Segerea , Hyness Petro Kanumba kutoka Rukwa, James Mangu (Mwanza), na Deborah Stanley mkazi wa Kimara kwa Komba jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati akikabidhiwa fedha zake za Ushindi, mshindi wa shilingi milioni 100 wa promosheni hiyo, Hamis Khalid, amewaomba Watanzania kutambua mchango mkubwa unaofanywa na Vodacom Tanzania katika kujenga na kuimarisha maisha ya Watanzania.
"Nimefuatilia Promosheni ya Jaymillions naona inalenga kuwakomboa kimaisha Watanzania hususani wenye kipato cha chini hasa wajasiriamali wadogo wadogo kama vile; wamachinga, mama ntilie, na pia wastaafu ambapo kwa kiasi kikubwa tunajua watu wa matabaka haya wanahitaji msaada ili kujiendeleza kiuchumi. Kwa fedha ambazo baadhi ya washindi tayari wamezipata wengi zimewasaidia kujikwamua na kujiendeleza kimaisha," alisema Khamis.
Aliongeza kuwa yeye ni mfano dhahiri wa Watanzania kuwa promosheni hii haina ujanja bali ya kweli kwa kuwa pamoja na kuishi mkoani ameweza kushinda na leo ameingiziwa fedha zake kwenye akaunti.
"Sasa nimepata mwanga katika maisha yangu baada ya kujishindia fedha hizi kwa sababu sijapewa masharti wala utaratibu wowote wa matumizi ya fedha hizi, maisha niliyokuwa nayo yalikuwa ya kuhangaika sana kutokana na kuwa na mtaji mdogo na sasa yamewezeshwa na promosheni hii’’.Alisema.
Khalid alisema kwa fedha hizi alizojishindia anaona tayari ameanza safari ya kuwa mfanyabiashara mkubwa mwenye mafanikio kwa kuwa ataimarisha biashara yake na kufungua miradi mbalimbali ikiwemo kusaidia familia yake ambayo inakabiliwa na changamoto mbalimbali za maisha.
Aliongeza kuwa ana matarajio ya kutoa msaada katika vituo vya watoto yatima kama njia yake ya kutoa shukrani kwa ushindi huu ambao umebadilisha maisha yake.
Akizungumza katika hafla iliyofanyika makao makuu ya kampuni hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia aliwahimiza wateja wote kuchangamkia promosheni ya JayMillions ili wajishindie mamilioni ya fedha kwa kuhakikisha wanatuma neno JAY kwenda namba 15544 ili kutopoteza bahati zao za kushinda.
Aliitaja njia nyingine ya kushinda kuwa ni kutuma neno AUTO kwenda namba 15544 iwapo simu haina fedha ambapo mteja akiweka fedha anakatwa shilingi 300/- tu.
“Tunaendelea kuwasisitizia wateja wetu wacheki kila siku ili kujua kama namba zao zimeshinda hasa kipindi hiki ambacho promosheni inaelekea ukingoni. Kama Khalid asingetuma ujumbe siku ile angeendelea tu na maisha yake kama yalivyokuwa bila kujua kama namba yake ilichaguliwa kushinda kwa maana bado kuna mamilioni ya kushinda yanayoweza kubadilisha maisha ya wateja wetu,” alisema Mworia.
Mbali na kumkabidhi zawadi yake nono hiyo, kampuni ya Vodacom inamsaidia Hamis kupata mafunzo ya ujasiriamali na matumizi sahihi ya ili kumuwezesha kufanya matumizi yenye tija.
No comments:
Post a Comment