Makamu wa Rais wa
kampuni ya StarTimes Tanzania, Bi Zuhura Hanif (kulia) akimkabidhi mshindi wa
droo ya kwanza ya kujishindia pikipiki ya mwezi wa Aprili, Bw Kafuku Mdaki,
mkazi wa Tanga, katika hafla fupi iliyofanyika katika duka la kampuni hiyo
zilizopo Bamaga-Mikocheni jijini Dar es Salaam. Kujiunga na bahati nasibu hiyo
wateja wa StarTimes wanatakiwa kulipia kifurushi kuanzia shilingi 10,000/- na
kuendelea.
Mshindi wa droo
ya kwanza ya kujishindia pikipiki ya mwezi wa Aprili inayoendeshwa na StarTimes
Tanzania, Bw Kafuku Mdaki, mkazi wa Tanga, akizungumza na waandishi katika
hafla fupi ya kukabidhiwa kwa zawadi yake katika duka la kampuni hiyo zilizopo
Bamaga-Mikocheni jijini Dar es Salaam. Kujiunga na bahati nasibu hiyo wateja wa
StarTimes wanatakiwa kulipia kifurushi kuanzia shilingi 10,000/- na kuendelea.
Mshindi wa simu akikabidhiwa simu yakeMteja akibonyeza kitufe cha kompyuta kumpata mshindi wa simu
Mteja akibonyeza kitufe cha kompyuta kumpata mshindi wa simu
Mteja akibonyeza kitufe cha kompyuta kumpata mshindi wa pikipiki
Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam, April 17, 2015.
STARTIMES Tanzania imemkabidhi mshindi wa droo ya kwanza ya kujishindia pikipiki Bw Kafuku Mdaki ambaye ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya English Medium ya Sir John iliyopo Bombo mkoani Tanga wakati wa kuchezesha droo ya pili bahati nasibu hiyo katika duka la kampuni hiyo lilipo Bamaga – Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa kukabidhiwa zawadi yake Bw Mdaki alibainisha kuwa hakuweza kuamini kama ni kweli amekabidhiwa zawadi hiyo kwani yeye huwa anajiunga na vifurushi vya mwezi kwa ajili ya kutazama na kufurahia vipindi vya kisimbuzi hicho na wala hakutarajia zawadi.
“Ni kweli nilikuwa na taarifa juu ya kuwepo kwa bahati nasibu hii na kwa bahati nzuri mimi huwa najiunga na vifurushi vya kila mwezi kwa ajili yangu binafsi na familia yangu, lakini bahati ikaniangukia mimi na kuwa mshindi. Kusema ukweli nimefurahi sana kwani pikipiki si zawadi ndogo tena ukizingatia unaipata bila ya kutarajia. Mawashukuru sana StarTimes kwa zawadi hii, kwa kweli mmenifanyia jambo jema kwenye maisha yangu.” Alisema Bw Mdaki
Akielezea ni kwa namna gani ataitumia pikipiki yake Mwalimu Mkuu huyo alisema kuwa, “Labda nizungumzie kwa upande wa sisi kule kwetu Tanga, pikipiki ni chombo muhimu sana kwa usafiri, kwa hiyo itanisaidia katika shughuli zangu binafsi na hata za kibiashara. Katika maisha ya siku hizi ukiwa na chombo cha usafiri basi unakuwa na uhkika wa kufanya shughuli zako bila ya wasiwasi. Kwani utakuwa na uhakika wa kwenda na kurudi bila ya kuhofia suala la kuchelewa ama kuwahi.”
“Ningependa kutoa wito kwa wateja wote wa StarTimes waamini kwamba bahati nasibu hii ni ya kweli na wala sio longolongo, hivyo waondoe shaka kama watakuwa wanatapeliwa. Pia kama mteja mzuri wa StarTimes napenda kuwapongeza kwa kuwa na huduma nzuri na zenye bei nafuu ambazo zinajali kipato cha watanzania walio wengi. Nawaomba waendelee kuboresha vipindi vyao, ili kukidhi haja za sisi wateja wao. Kwa mfano mimi napenda sana michezo na nafurahia nikiona baadhi yake ikiwemo kwenye kisimbuzi hiki.”
Naye kwa upande wake Makamu wa Rais StarTimes Tanzania, Bi Zuhura Hanif alitoa pongezi zake za dhati kwa mteja huyo wa kwanza wa droo ya bahati nasibu ya kujishindia pikipiki na kuwataka wengine walipie kwani wanaweza kuwa washindi bado zoezi linaendelea.
“Kwanza kabisa kwa niaba ya kampuni na wafanyakazi wote ningependa kuchukua fursa hii kumpongeza mshindi wetu wa kwanza wa pikipiki pamoja na washindi wengine wa simu za mkononi za kisasa. Mshindi huyu alipatikana kwa kulipia kifurushi chake cha mwezi na nawasihi wengine nao wafanye hivyo. Kwa malipo ya kuanzia shilingi 10,000 tu unapata faida ya kufurahia chaneli na vipindi vyetu vizuri na huku ukisubiria bahati ya kuibuka na pikipiki na zawadi zingine.” Alisema
“StarTimes inafanya haya yote ikiwa ni jitihada za kuwajali na kuwakumbuka wateja wake kwani wao ndio wadau wao wakubwa katika biashara. Kwa kuonyesha kuwa tunawajali ningependa kuwadokezea wateja wetu na watanzania kwa ujumla kuwa kuna maboresho makubwa ya chaneli na vipindi vyetu yatafanyika kuanzia mwezi huu wa Aprili na kuendelea. Kuna vipindi na chaneli za kuvutia kuhusu michezo, filamu, watoto, dini na kadhalika zitaongezwa hivi karibuni.” Aliongezea
“Mbali na hapo pia tunatarajia kuwa tutafanya punguzo la bei la visimbuzi vyetu vya antenna za nje na dishi. Lengo la kufanya hivi ni kuendeleza na kudhihirisha dhamira yetu ya kuifanya kila nyumba ya mtanzania kuwa na uwezo wa kupata matangazo ya luninga kwa dijitali yaliyo bora na kwa bei nafuu katika siku chache zijazo hivyo mkae mkao wa kula. Asanteni na kwa mara nyingine tena niwapongeze washindi wa droo ya kwanza waliokabidhiwa zawadi zao leo na wale waliopatikana katika droo hii ya pili.” Alihitimisha Bi Hanif
Mshindi wa droo ya pili ni Bi Janemerry Suraphel, mkazi wa Dar es Salaam, alipatikana katika droo ya bahati nasibu iliyochezeshwa mbele ya waandishi wa habari na wateja waliopo dukani hapo.
Mbali na mshindi huyo droo ya kwanza aliyekabidhiwa pikipiki pia kulikuwa na washindi wengine nane kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania ambao walijishindia simu za kisasa kutoka StarTimes ikiwa ni kama zawadi kutoka kwa kampuni kwenda kwa wateja wake. Simu hizo zilizoenda kwa washindi ni Solar 5 nne na P40 nne.







No comments:
Post a Comment