TANGAZO


Sunday, April 19, 2015

Maadhimisho ya Siku ya Hedhi Duniani yanakaribia

*Girl Pawa’ yafanikiwa kupunguza utoro wa wasichana  Mtwara.

Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (Kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati alipokuwa akimtangaza mshindi wa shilingi milioni 100  mwishoni mwa wiki kupitia promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na kampuni hiyo, ambapo Irene Mrema mkazi wa Kawe jijini Dar es Salam,(30) alijishindia kitita hicho.Kushoto ni Afisa Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Nchini Jehud Ngolo.Ili  mteja kujua kama  ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544. 
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (Kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati alipokuwa akimtangaza mshindi wa shilingi milioni 100  mwishoni mwa wiki kupitia promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na kampuni hiyo, ambapo Irene Mrema mkazi wa Kawe jijini Dar es Salam,(30) alijishindia kitita hicho.Kushoto ni Afisa Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Nchini Jehud Ngolo.Ili  mteja kujua kama  ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.

Wakati maadhimisho ya siku ya hedhi duniani Mei 28 yanakaribia ambayo taasisi na wadau mbalimbali duniani huitumia kuzungumzia changamoto za kipindi cha hedhi kwa watoto wa kike na namna ya kuzikabili, hapa nchini mradi wa Hakuna Wasichoweza unaotekelezwa na taasisi ya T-MARC chini ya ufadhili wa Vodacom Foundation na USAID umeonyesha mafanikio makubwa katika awamu ya kwanza kwa kupunguza utoro wa wasichana mashuleni wanapokuwa katika vipindi vya hedhi.
Lengo la Mradi wa Hakuna Wasichoweza  ni kuwapatia elimu ya uzazi,afya,kuwajengea uwezo wa kujiamini na kuwapatia Pedi za gharama nafuu watoto wa kike waliopo katika umri wa kuvunja ungo na umeanza kutekelezwa mkoani Mtwara lengo likiwa ni kutekelezwa katika mikoa mbalimbali ya Tanzania katika siku za usoni.
Meneja wa mradi huu wa T-MARC,Doris Chalambo amesema kuwa idadi ya wasichana wanaohudhuria masomo mashuleni imeongezeka tofauti na siku za nyuma ambapo wasichana walipokuwa wanaingia katika hedhi wengi wao walikuwa wanashindwa kuhudhuria kwenye masomo kutokana na kutokuwepo na mazingira rafiki ya kukabiliana na hali hiyo .
Shariffa Khamis mmoja wa wanafunzi wa shule ya Mwenge mkoani Mtwara ambaye amenufaika na mradi huu akitoa ushuhuda kwa niaba ya wenzake ni kwa jinsi gani wasichana wenzake zaidi ya 5,000 wamenufaika na mradi huu alipohojiwa hivi karibuni alisema”Sasa nafurahia masomo yangu ikiwemo maendeleo yangu darasani kuwa mazuri darasani.

Najisikia vizuri kuwa mwanafunzi.Natamani mradi wa Hakuna Wasichoweza  ungeanza kitambo.Hata  hivyo naona mabadiliko makubwa ya kumuwezesha mtoto wa kike na kumjengea uwezo wa kujiamini yanakuja tukiendelea na kasi hii…”
Mwanafunzi Sharifa alikiri kuwa tangu kuanzishwa kwa mradi wa Hakuna Wasichoweza maarufu kama Girl Power mahudhurio ya wasichana shuleni kipindi chote cha masomo yameongezeka pia ufanisi wao katika masomo umeongezeka kwa kiasi kikubwa tofauti na ilivyokuwa hapo awali na wamepata ufahamu juu ya ugonjwa wa UKIMWI na magonjwa mengine ya zinaa na madhara ya mimba za utotoni.
Maneno hayo yaliungwa mkono na Mwalimu Monica Mfaume wa shule hiyo  aliyekuwepo wakati ukitolewa ushuhuda huo.
Jamila Issa mwanafunzi mwingine aliyenufaika na mradi huu alitoa ushuhuda kwa kuajiamini akisema: “Mradi huu ni mzuri na unaleta faraja kwa watoto wa kike kwa kuwa unawajengea uwezo kwa kuwapatia elimu ya afya na uzazi na jinsi ya kuepuka kujihusisha na ngono zisizo salama pia unatoa elimu ya kujitunza wakati wa kipindi cha hedhi”.
Aliendelea kusema kuwa pia hatua ya kuwapatia wasichana Pedi inasaidia wanafunzi wengi wa kike kuendelea na shughuli zao wanapokuwa katika kipindi hicho ikiwemo kuhudhuria masomo yao shuleni kama kawaida.

Jamila anakiri kuwa  sehemu za vijijini kumekuwepo na changamoto za wasichana kupata Pedi za kuwasaidia wanapokuwa kwenye hedhi na zinapopatikana zinakuwa na bei kubwa wasizoweza kumudu hali inayosababisha wawe wakitumia njia zisizo salama za kujikinga.
 Kutokana na mafanikio yaliyopatikana katika awamu ya kwanza ya mradi wa kuwawezesha wasichana wa Hakuna  Wasichoweza,taasisi ya Vodacom Foundation imeongeza ufadhili wa Dola za Kimarekani 166,000 ili mradi uendelee na uweze kuwafikia wasichana 4,200 katika shule nyingine 10 katika mkoa wa Mtwara.
Mkuu wa Vodacom Foundation Reenu verma amesema : “Vodacom Foundation kupitia mradi wake wa Girl Pawa imelenga kuwawezesha wasichana na wanawake kutimiza ndoto za maisha yao kwa kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowafanya  wabaki nyuma baadhi yake zikiwa ni ukosefu wa elimu na kutojiamini na tumeamua kuongeza ufadhili ili mradi uweze kuwafikia wasichana wengi zaidi”
Awamu ya kwanza ya mradi huu ilifadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID) ambalo lilitoa ufadhili wa Dola za Kimarekani 200,000 na taasisi ya Vodacom Foundation ambayo ilitoa Dola za Kimarekani 100,000 na umenufaisha zaidi ya wasichana 5,000 ambapo katika awamu ya pili unategemewa kunifaisha wasichana wengi zaidi.

No comments:

Post a Comment