Mchungaji wa mifugo akinywesha maji mifugo yake kwenye eneo
lenye maji ambalo Waizri Prof. Maghembe amepiga marufuku kunywesha kwenye eneo
hilo.
Na Hussein
Makame-MAELEZO, Musoma
WAZIRI wa
Maji Profesa Jumanne Maghembe amewaonya wananchi wanaoharibu vyanzo vya maji
kwamba kufanya hivyo kunahatarisha uhai wa vyanzo hivyo.
Ametoa
onyo hilo kwa nyakati tofauti wakati
akiwa kwenye shughuli za kuweka mawe ya
msingi kwenye miradi ya maji kwenye maeneo mbalimbali ya wilaya ya
Serengeti mkoani Mara ambako Maadhimisho ya Wiki ya Maji kitaifa yanafanyika.
Akiwa katika
kijiji cha Rung’abure, Waziri alishuhudia baadhi ya wafugaji wakinywesha mifugo
yao kwenye maeneo ya vyanzo vya maji huku baadhi wakilima karibu na chanzo cha
maji.
“Jamani
mradi huu ni wa kwenu, lakini nilichokiona pale kwenye chanzo cha maji, nilina
ng’ombe kwenye eneo chepechepe” alisema Waziri Prof. Maghembe na kungeza:
“Jamani
fanyeni juhudi au lolote mnalofanya lakini msiingizi ngombe mule kama mkiingiza
basi maisha ya mradi yatakuwa mafupi na hakuna mtu wa kumlaumu kwa sababu ni nyinyi
wenyewe mmekuwa kama mtu anayekata tawi la mti alilokalia”.
Aliongeza
kuwa katika eneo la mradi wa Rung’abure kuna mkulima analima kwenye msitu
ulioko karibu na chanzo cha maji cha mradi wa kijiji hicho, hivyo anahatarisha
chanzo hicho.
“Mtu yule
tunamuomba mwaka huu avune mazao yake lakini mwaka kesho asipande pale.Mwenyekiti
naomba mumpe shamba lingine kwa sababi akiendelea kulima hakuna maji pale”
alisema Waziri Prof. Maghembe.
Alifafanua
kuwa suala la kuondoka si hiyari kwani
hairuhusiwi kisheria kulima mita 60 kutoka chanzo cha maji, hivyo mkulima huyo
ni lazima aondoke mwakani.
“Hili jambo
ninalosema si hiari ni suala la kisheria hairuhusiwa kulima kwenye chanzo cha
maji kwa umbali wa mita 60 na hilo sio jambo la kumuomba mtu ni jambo la
kutekeleza sheria” alisema na kuongeza:
“Ninachosema yule aliyelima pale mwaka huu avune
mazoa yake mi sina tatizo kabisa baada ya hapo tunamuoba aondoke pale sheria
hii sio ya mwaka huu, wala mwaka jana wala mwaka juzi na hilo ni sheria imetungwa
mwaka ya 2006”.
Aliitaka
Serikali ya kijiji hicho pia wanasimamia kuhakikisha ng’ombe hawapelekwi kunywa
maji kwenye eneo la chanzo cha maji badala yake wakanywe maji kwenye mabirika
yaliyojengwa.
Akiwa mjini
Mugumu wilayani Serengeti, ambako alitembelea ujenzi wa chujio la maji ya bwawa
la Manchira na baada ya ukaguzi huo alizungumza na wananchi wa mji huo.
Alisema chujio
hilo litachuja maji na kuweka dawa kwenye maji yanayokwenda mjini na kutatua
tatizo la uchafu wa maji ambalo linawakabili wananchi wa Mugumu.
“Lakini pia
niwaombe sana ndugu zangu mtunze sana mazingira kwani tumeona rasilimali za maji zinapungua sana
ninawaomba mtunze sana vyanzo vya maji mtunze na bwawa letu la Manchira”
alisema Waziri Prof. Maghembe.
Hivyo
alisisitiza kuwa ili kuhakikisha bwawa hilo na linaendelea kutumika kwa kipindi
kirefu, kitu kikubwa ni kutunza sana mazingira ili kiasi cha rasilimali kilichopo
kisiendelee kupungua.
Akiwa katika
vijiji vya Ligamba A na Mumagunga vilivyoko wilayani Bunda mkoani Mara, Waziri
aliwataka wananchi wapande miti ili kulinda vyanzo vya maji kwenye maeneo yao.
Alisema
utunzaji wa vyanzo vya maji ni jambo muhimu ili kuhakikisha kuwa vyanzo vya
maji havikauki na kujharibiwa kwani kufanya hivyo kutahatarisha upatiakanaji wa
maji.
Waziri Prof.
Maghembe anaendelea na ziara ya kukagua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi
ya maji katika vijiji mbalimbali vya wilaya za mkoa wa Mara ikiwa ni sehemu ya
Maadhimisho ya Wiki ya Maji Kitaifa.
No comments:
Post a Comment