TANGAZO


Tuesday, March 24, 2015

Wateja Duka la Woolworths kununua kwa nusu bei Pasaka

Meneja Masoko wa maduka ya Woolworths Tanzania,Edwina Barongo akisisitiza jambo kwa wateja waliofika katika Uzinduzi wa punguzo la bei ya bidhaa zote zinazouzwa katika Maduka yote ya Woolworths yaliyopo Arusha na Dar es Salaam, Punguzo hilo litadumu kwa muda wa wiki Nne ikiwa ni sehemu ya kusherehekea sikukuu ya Pasaka.Hafla hiyo ilifanyika  jijini Dar es Salaam jana.
Meneja Mkuu wa kampuni ya Woolworths Tanzania, Joehans Bushiri akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa punguzo la bei kwa bidhaa zinazouzwa katika maduka yote ya Woolworth, kwa kipindi cha wiki Nne ikiwa ni sehemu ya ponguzo  la kununua bidhaa bora kwa kipindi hiki cha sikukuu ya Pasaka.Hafla ya uzinduzi ilifanyika jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi (Loyal Customer) Manfred Ngantunga (kulia) akizindua duka la Woolworths  lililopo mtaa wa Ohio jengo la PPF Tower ikiwa ni sehemu ya kuzindua punguzo la bei nafuu kwa bidhaa zinazouzwa na kampuni hiyo katika maduka yaliyopo Arusha na Dar es Salaa.Katikati ni Meneja Mkuu wa Woolworths Tanzania Joehans Bushiri na Mkurugenzi wa fedha Samson Katemi(kushoto).Uzinduzi huo wa Punguzo la bei kwa asilimia 50 utadumu kwa muda wa wiki Nne ulifanyika jijini Dar es Salaam.
Mteja wa muda mrefu wa  bidhaa zinazouzwa  kwenye maduka ya Woolworths (Loyal Customer) Manfred Ngantunga  (kulia) ambaye alikuwa mgeni rasmi  na Meneja Mkuu wa Woolworths Tanzania Joehans Bushiri  wakiingia ndani ya duka hilo mara baada ya uzinduzi wa punguzo la bei la bidhaa zinazouzwa katika maduka hayo.Kushoto ni Mkurugenzi wa fedha Samson Katemi hafla hiyo ya Punguzo la bei kwa asilimia 50 ilifanyika  jijini Dar es Salaam  itadumu utadumu kwa muda wa wiki nne.
Mteja wa muda mrefu wa  bidhaa zinazouzwa kwenye maduka ya Woolworths ambaye pia alikuwa Mgeni rasmi Manfred Ngantunga (katikati)  akikabidhiwa zawadi na mfanyakazi wa duka hilo, baada ya kuzindua punguzo la bei la bidhaa kwa asilimia 50%zinazouzwa kwenye maduka ya hayo Tanzania, Kulia ni Meneja Mkuu wa Woolworths Joehans Bushiri,Hafla ya uzinduzi ilifanyika makao makuu ya woolworths  jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya wateja wa wakinunua bidhaa mbalimbali zinazouzwa katika duka la  Woolworths lililopo jijini Dar es Salaam, mara baada ya uzinduzi wa punguzo la bei litakaloduma kwa wiki Nnne kwa maduka yote nchini kwa asilimia 50% kwa bidhaa zote zinazouzwa katika maduka yote ya Woolworths yaliyopo jijini Arusha na Dar es Salaam.
Baadhi ya wateja wa wakinunua bidhaa mbalimbali zinazouzwa katika duka la  Woolworths lililopo jijini Dar es Salaam, mara baada ya uzinduzi wa punguzo la bei litakaloduma kwa wiki Nnne kwa maduka yote nchini kwa asilimia 50% kwa bidhaa zote zinazouzwa katika maduka yote ya Woolworths yaliyopo jijini Arusha na Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu         
Katika pindi hiki cha sikuu ya Pasaka watanzania wanaweza kununua nguo zenye ubora kwa nusu bei kufuatia punguzo la silimi 50 lililotangazwa jana na duka maarufu la nguo la Woolworths jijnini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa punguzo hilo, mkurugenzi wa duka hilo Joehans Bushiri aliawambia wateja waliofika dukani hapo kuwa punguzo hilo titadumu kwa muda wa wiki nne.

Alisema lengo kubwa la Woolworths ni kuwawezesha watanzania wenye vipato  vya aina mbali mbali kufurahia sikukuu ya Pasaka kwa kupata nguo za kisasa zenye ubora kwa gharama nafuu.

Mkurugenzi huyo pia aliwaasa watanzania kuachana na nguo za mtumba“Tunawasihi watanzania kuepukana na matumizi ya nguo za mtumba kwani si salama kwa afya zao. Katika kipindi hiki cha sikukuu ya Pasaka duka la Woolworths linatoa punguzo kubwa ili kuwawezesha watanzania kupata nguo mpya na zenye ubora.,” alisema.
Bushiri alisema duka hilo ambalo ni moja kati ya maduka makubwa ya nguo hapa nchini, litaendelea kuwahudumia wateja wake kwa kuwaletea nguo nzuri na zenye ubora kwa gharama nafuu na hivyo kuwasaidia kuepukana na nguo za mtumba.

“Mteja anayekuja kununua nguo dukani kwetu anakuwa amefanya uamuzi sahini kwani atapa nguo zenye ubora kwa gharama nafuu na atakuwa amepata kitu ambacho kinaendana na thamani ya pesa yake,” alieleza.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa, duka hilo pia linatoa nafasi kwa wateja kununua nguo kwa kulipia kidogo hadi kwa muda wa miezi mitatu ili kuwawezesha wale wasio na fedha za kutusha kulipa mara moja kuweza kufurahia nguo zenye ubora.

Kuhakikisha wateja wetu wanapata vitu bora kabisa, vinavyoendana na wakati na kwa mda muafaka, Woolworths imeweza kubadilisha mfumo wa uletaji wa bidhaa nchini badala ya kutumia meli kama zamani sasa inatumia usafiri wa ndege. 

Kabla ya hapo tulikuwa tun kunatumia muda wa mwezi mmoja hadi miwili kufikisha mizigo nchini wakati kwa sasa tunatumia mda wa wiki mbili hadi tatu.

Bwana Bushiri pia akasisitiza kwamba anapenda kuwahakikishia wateja wao kwamba Woolworths Tanzania ina bidhaa zote kama zinazopatikana South Africa na kwa bei zinazofaa kabisa. 

Kwa upande wake Manfred Ngatunga ambaye ni mmoja kati ya wateja wazuri wa duka hilo alitoa shukrani zake kwa uongozi wa duka hilo kwa kutoa punguzo kubwa haswa katika mismu huu wa sikuu ya Pasaka.

Uamuzi wa punguzo la bei umekuja kipindi kizuri sana. Kipindi hiki na kipindi ambacho familia zinafanya manunuzi kwa ajili ya sikuu ya Pasaka. Tunashukuru kwa kuwa tutapata nguo zenye ubora kwa nusu bei, kila mtu sasa anaweza kupendeza,” alieleza

No comments:

Post a Comment