Mhandisi wa Maji Wilaya ya Serengeti Marwa Mulaza(kushoto aliyesimama), akisoma taarifa ya mradi wa Maji wa kijiji cha Nyagasense mbele ya Mgeni Rasmi Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe.
Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nyagasense baada ya kuweka jiwe la Msingi na kutembelea mradi wa maji wa kijiji hicho.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Nyagasense wakimsikiliza Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe (hayupo pichani).
Mkazi wa kijiji cha Nyagasense Christina Machota akiuliza swali kwa Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe
Mkutano wa Waziri na wananchi wa kijiji cha Nyagasense ukiendelea.
Sehemu ya wananchi wa kijiji cha Nyagasense wakimsikiliza Wazari Prof. Maghembe.
Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe, akiwa ameambatana na wenyeji wake wakielekea kukagua chanzo cha mradi wa Maji wa kijiji cha Rung’abure.
Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe, akikagua bwawa la maji ya Mradi wa Maji wa kijiji cha Rung’abure.
Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe, akiweka jiwe la msingi kuzindua Mradi wa Maji wa kijiji cha Rung’abure.
Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe (katikati), akikagua miundombinu ya mradi wa maji wa Rung’abure.
Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe, akionja maji ya mradi wa maji wa kijiji cha Rung’abure.
Kijana aliyekutwa akinywesha maji mifugo yake kwenye chanzo cha maji cha mradi wa maji wa Rung’abure.
Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe, akikagua tenki la maji la mradi wa maji wa Rung’abure.
Diwani wa Kata ya Rung’abure Ezekia Binagi akimkaribisha Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe, kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Rung’abure(katikati) na kulia ni Mwenyekiti wa kijiji hicho Marwa Joseph Meng’anyi.
Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Rung’abure (hawapo pichani).
Mmoja wa
wananchi wa kijiji cha Rung’abure akiuliza swali Waziri wa Maji Prof. Jumanne
Maghembe, wakati wa mkutano wake na wananchi hao.
Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe, akizungumza na
wananchi wa kijiji cha Rung’abure. (Picha
zote na Hussein Makame-MAELEZO, Musoma)
Na Hussein
Makame-MAELEZO, Musoma
WAKAZI wa
vijiji viwili vya Nyagasense na Rung’abure vilivyoko kwenye Wilaya ya Serengeti
mkoani Mara, wamehakikishiwa kuanza kupata maji ifikapo mwishoni mwa wiki hii
kufuatia wakandarasi wanaojenga miradi ya maji ya vijiji hivyo kuahidi
kufikisha maji katika kipindi hicho.
Akitoa ahadi
kwa Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe wakati wa mkutano wake na wananchi
wa kijiji cha Nyagasense, Mhandisi wa mradi wa maji wa kijiji hicho John Mapande
amesema maji yataanza kutoka siku tatu kuanzia leo.
Mhandisi
Mapande alitoa ahadi hiyo wakati Waziri Prof. Maghembe akizungumzia matumaini
ya kukamilika kwa mradi huo wa maji ambapo aliwaomba wananchi wa kijiji hicho
kukaa mkao wa kunywa maji.
“Ninawomba
sana mkae mkao wa kunywa maji kwa sababu nimeona kwa macho yangu na nimeridhika,
vinginevyo nisingeweka jiwe la msingi, hivyo katika kipindi kifupi maji
yatafika huku mitaani” alisema Waziri Prof. Maghembe.
Baada ya
kutoa matumaini hayo, Waziri Prof. Maghembe alimuita mkandarasi wa mradi huo na
kumsihi kukamilisha mradi huo na kwamba fedha zake zilizobaki atalipwa, na
mazungumzo yao yailikuwa hivi:
Waziri:
Mkandarasi uko wapi?
Mkandarasi:
Niko hapa mheshimiwa Waziri.
Waziri: Sasa
wewe ukamilishe mradi wangu, ile miezi sita ikiisha fedha zako zitakazokuwa
zimebaki tutakulipa, kwa hiyo we maliza mradi haraka wiki ijayo mimi ninywe
maji hapa kabla sijakwenda Dar es Salaam.
Mkandarasi: Nitajitahidi
Mhe Waziri kukamilisha.
Waziri:
Jitahidi, maana kazi iliyobaki ni kidogo sana kukamilisha huu mradi
Mkandarasi: Ni
kazi ya siku mbili au siku tatu maji yatakuwa yameshatoka
Waziri: Eeh
sasa kazi ya siku mbili tatu mimi nitakuwa Mara hapa, nataka nikienda Mugumu
nisimame hapa ninywe maji.
Kwa upande
wa mradi wa Maji wa kijiji cha Rung’abure, Waziri Prof. Maghembe alimuagiza
mkandar akafunge jenereta na kupeleka pampu na kuifunga ili maji yaanze
kusukumwa kuanzia leo.
Waziri Prof.
Maghembe alichukua hatua hiyo kutokana na baadhi ya wananchi kuzuia malori
yanayopeleka jenereta na pampu kwenye eneo la mradi, kupita kwenye eneo lao,
lakini Serikali ya kijiji ilimuhakikishia Waziri kwamba wananchi hao wameruhusu
gari ipite.
Waziri: bwana
mkadarasi yuko wapi
Mkandarasi: Nipo
hapa mheshimiwa
Waziri: Nimemuagiza
huyu mkandarasi kesho alete jenereta ifungwe kwenye nyumba ya genereta na alete
pampu pale ifungwe ili maji yaanze kusukumwa kesho.
Kwa hiyo
muangalie atafunga kesho labda jioni atakuwa amekamilisha, lakini hata kama
hakukamilisha Alhamisi atakamilisha, Alihamisi akikamilishwa bado nitakuwa mkao
wa Mara.
Kwa hiyo
siku ya Alhamisi kwa uhakikka wataanza kusukuma maji, nimeona kazi nyingi hazijakamilika,
lakini hiyo ikamilishwe kesho na Alhamisi ili sasa wakati wanaendelea na kazi
nyingine mnaendelea kunywa maji.
Baada ya
kuzungumza hayo, wananchi walipiga vigelegele na makofi kuonesha kufurahishwa
na hatua hiyo.
Wakizungumza
kufurahishwa na matumaini hayo ya kupata maji, baadhi ya wakazi wa kijiji cha
Nyagasense wamesema wamefurahi kupata ujio wa Waziri na hatimaye kuahidiwa
kupata maji.
“Kwa kweli tumefurahi
sana kupata ujio wa Waziri wa Maji na tumeridhika na ahadi ya kupata maji wiki
hii kwa sababu tumekosa maji kwa miaka miwili sasa tulikuwa tunapata shida ya
kuyapata” alisema mkazi wa kijiji hicho Christina Machota.
Mradi wa
Maji wa kijiji cha Nyagasense unaotekelezwa chini ya Programu ya Maji na Usafi
wa Mazingira, unatumia chanzo cha kisima kirefu chenye uwezo wa kutoa maji lita
6000 kwa saa na utakapo kamilika utahudmia watu 5,530 na mifugo 2620.
Mradi huo
una jumla ya kilometa 19.54 za mtandao wa mabomba ya maji na vituo 20 vya
kuchote maji na birika 2 za kunyweshea mifugo.
Akiwasilisha
taarifa ya mradi wa maji wa Rung’abure, Mhandisi wa Maji Wilaya ya Serengeti
Marwa Mulaza, alisema una chanzo cha maji mtiririko na hutoa lita 10,000 kwa
saa na ulianza kutekelezwa Oktoba mwaka2013.
Alisema
mradi huo utakapokamilika utahudumia watu 3, 457 na mifugo na unatarajiwa
kukamilika tarehe 30 Aprili mwaka huu 2015.
No comments:
Post a Comment