TANGAZO


Monday, March 16, 2015

Maabara ya kiuchunguzi ya ebola

*Serikali kujenga maabara za magonjwa ya mlipuko
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii, Dkt. Steven Kebwe.

Na Catherine Sungura, MOHSW-Ndanda
SERIKALI imedhamiria kujenga na kuboresha maabara za kiuchunguzi za magonjwa ya Milipuko ili kupunguza gharama za usafirishaji sampuli nchi jirani.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii, Dkt. Steven Kebwe wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa maabara ya kisasa kwenye hospitali ya mtakatifu benedict iliyopo ndanda.

Alisema Lengo la ujenzi wa maabara hizo ni kurahisisha shughuli za kiuchunguzi wa magonjwa ya Milipuko nchini yanayoweza kutokea katika mikoa ya Kanda ya Kusini.

"awali tulikuwa tukipata taarifa ya mtu anayehisiwa na moja ya magonjwa ya Mlipuko Ilikua tunachukua sampuli ya damu na kuisafirisha nchini Kenya ama afrika ya Kusini,hivyo kama serikali ilitugjarimu sana.

Aidha alisema wizara kupitia ubadilishe wa Benki ya Dunia inatarajia kujenga maabara ya kitaifa ambayo itaunganisha maabara zote nchini zilizomo kwenye mpango wake
Dkt. Kebwe alisema maabara hiyo itagharimu kiasi cha shilingi za kitanzania billioni 1.04 ambapo litakua ni la sakafu ya moja(ghorofa moja) Ila kwa kuanza serikali itajenga sakafu ya chini.
Ujenzi wa Maabara hiyo inatarajiwa kukamilika mapema mwaka ujao chini ya wizara ya afya na ustawi wa jamii
Alitaja magonjwa ya Mlipuko ni pamoja na ebola,dengue,chipungunya na murmur.

No comments:

Post a Comment