Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Joshua Mirumbe akisoma taarifa ya Sekta ya Maji ya wilaya yake kwa Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe.
Mtendaji wa Kijiji cha Ligamba A, Debora Faresi akisoma taarifa ya Mradi wa Maji wa Ligamba/Kitaramaka.
Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe, akiweka jiwe la msingi la Mradi wa Maji wa Ligamba/Kitaramaka.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watumiaji Maji kijiji cha Mumagunga, Wegoro Chikoba, akisoma taarifa ya Mradi wa Maji wa kijiji hicho.
Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe, akiteta jambo na Mbunge wa Mwibara Kangi Lugola.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mumagunga Francis Kazimoto, na akipokea hati ya makabidhiano ya Mradi wa Maji wa Mumagunga, na Mkandarasi wa Mhandisi wa Kampuni ya Ukandarasi ya Halem Co Ltd, Mhandisi Juma Msasa.
Mbunge wa Mwibara Kangi Lugola, akizungumza na wananchi wa kijiji huku akionesha furaha yake kwa Waziri wa Maji, Prof. Maghembe.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mumagunga, wakieleza furaha yao kwa kupata maji.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mumagunga, wakieleza furaha yao kwa kupata maji.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mumagunga, wakieleza furaha yao kwa kupata maji.
Hussein
Makame-MAELEZO, Bunda
WANANCHI wa
Vijiji vya Ligamba A na Mumagunga wameishukuru Serikali kwa kuwapatia huduma ya
maji kwani ndoa zilianza kuparaganyika na kwamba itaepusha watoto wa nje ya
ndoa kutokana na wanaume kukosa muda wa kukaa na wake zao kwa kuhangaikia maji.
Wameleza
hayo baada ya Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe kuweka mawe ya msingi
kwenye miradi ya maji ya vijiji vyao ambayo itawafanya wapate maji ambayo
walikuwa wakiyakosa kwa muda mrefu.
Wakizungumza
kwenye mkutano wa kijiji cha Mumagunga, baadhi ya wananchi wa kijiji hicho
wamesema wamekuwa wakihamka saa 8: 00 usiku kwenda kutafuta maji huku
wakiwaacha waume zao nyumbani na wakati mwingine kurejea bila maji.
“Kwa niaba
ya kina mama wa kijiji cha Mumagunga napenda kumshukuru Waziri kwa kupata
nafasi ya kufika hapa kwetu leo, ni farijiko la kina mama wa Mumagunga kwa mara
ya kwanza tumumuona Waziri hapa kijijini kwetu” alisema Milta Masau na
kuongeza:
“Lakini pia
tunapenda kushukuru mradi kufika hapa kwetu na wakina mama wa Mumagunga
tumekuwa tukipata adha ya siku nyingi na tumekuwa tukihangaika kwa muda mrefu
sana.Utakuta mama anaamka asubuhi saa 12 kwenda kutafuta maji lakini mpka saa 9
ndio anafika nyumbani huku hajapata maji”
Alisema hali
hiyo ilisababisha familia zetu ziki[ata shida ni namna gani ya kupata huduma za
kila siku lakini sasa kutokana na kupelekewa mradi huo adha hiyo itakuwa
umeondoka.
Naye Lucia
Mahela alishukuru kwa kupata maji kwani
walikuwa na shida sana na huduma hiyo kwani walikuwa wakiamka asubuhi sana na
wakati mwengine walipigana na waume zao kutoakana na kukosa huduma hiyo.
“Tunashuku
mbunge wetu kwa kupata maji kwa sababu tulikuwa tunamka saa 8 usiku kutafuta
maji na saa nyingine tunarudi bila maji na tunapigana kwa ajili ya maji, lakini
leo tumenenepa kwa ajili ya maji” alisema Mahela na kuongeza:
"Msinione
kukonda hivi ni kwa ajili ya maji nafikiri baada ya muda wa wiki moja nitakuwa
nimeshanenepa.Sasa mimi naomba kwa wenzangu huyu (mbunge) tumfanye mkono
aendelee mpaka mwisho”
Kwa upande
wao Wilison Mlengwa na Yahya Gngemka walishukuru kupata maji kwani wake zao
walikuwa wanawaacha vitandani kwenda kutafuta maji na hali hiyo itaepusha
kupata watoto nje ya ndoa.
“Nishukuru
ujio wa Waziri wa Mji Profesa Jumanne Maghemba na mbunge wetu Kangi Lugola kwa
jitihada kubwa, nisememe kwamba kwa muda mrefu tulikuwa na shida ya maji lakini
leo tumepata nuru” alisema Lmengwa na kuongeza:
“Na hata
wake zetu watapata kupumua kwa sababu siku nyingi tulikuwa wanatuacha kwenye
vitanda wanaenda kwenye maji na tutakuwa nao bega kwa bega mpaka asubuhi”.
Naye
Gengemka alishukuru kupata maji kwani ndoa zo zilishaanza kuparaganyika kwa
sababu ya shida ya maji.
“Kwanza
nashukuru kupata maji tulikuwa na matatizo mengi ndoa zetu pia zilikuwa
zimeanza kuparaganyika kwa sababu zilikuwa zinaonekana nusu siku, robo siku
tulikuwa tunakaa na wanawake” alisema na kuongeza:
“Kati ya saa
12 usiku tulikuwa tunakaa saa 3 tu, asaa zaidi zilikuwa ni kuhemea maji, kwa
hiyo sasa hivi nashukuru kwamba ndoa zimezidi kuimarika kwa hiyo hatutakuwa na
matatizo tena ya watoto ambao wapo kinyume na utaratibu wa ndoa”
Wananchi wa
kijiji cha Ligamba walisema tatizo la maji timewasababishia matatizo makubwa
katika ndoa zao, hivyo kuwekwa jiwe la msingi ni matumaini kuwa watapata maji
ya inavyotarajiwa.
Mbunge
Lugola alikiri kumsumbua sana Waziri Prof. Maghembe juu ya huduma ya maji kwa
wananchi wake lakini alimuomba amuamini kwamba maji yatapatikana na yeye
angekwenda, na kweli ameona.
Alisema
tatizo hilo la maji lilisababisha wanawake wa Mumagunga wakipata posa
wanakataliwa kutokana na tatizo la maji, hivyo anashukuru kwa jitihada zake za
kuwapatia maji.
Waziri wa
Maji Prof. Maghembe alioneshaKarukekere mradi umekamilika na Mramba mradi
umetekelezwa kwa asilimia 70 ambayo asilimia iliyobaki itakamilishwa kwa
asilimia 100.
Alisema
mradi huo sasa ni wa kijiji hivyo wauendeshe kwa kufuata taratibu na kuzingatia
utoa matunda ya kutosha kwa wananchi wa kijiji hicho na wala wasifanye mradi
huo kuwa biashara.
No comments:
Post a Comment