*Ni kwenye tamasha la maisha murua la Vodacom
*Prof J,Chege,Temba na magwiji wengine kupanda jukwani
WAPENZI
wa burudani ya muziki wa kizazi kipya watapata burudani ya fungua
mwaka kutoka kwa magwiji wa muziki
wa kizazi kipya ambao wanatamba nchini katika tamasha la wazi la
maisha murua na Vodacom katika ufukwe wa Coco beach jijini Dar es
Salaam.
Baadhi ya magwiji hao ni
Profesa J, Temba, Chege, Roma Mkatoliki na wengineo wengi.
Tamasha hili litakalokutanisha magwiji wa bongo fleva ambalo limeanza kuwa gumzo la jiji kutokana na kuwa na
burudani za aina mbalimbali kwa ajili ya kukonga nyoyo za wapenzi wa burudani limeandaliwa na Vodacom Tanzania.
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu amesema kuwa Vodacom imeamua kuandaa tamasha hili la”Vodacom
Maisha ni Murua” kwa ajili ya kuwapatia furaha na burudani wateja
wake na wananchi kwa ujumla katika sikukuu ya mwaka mpya vilevile
wananchi watapata fursa ya kujinunulia bidhaa mbalimbali za huduma za
Mawasiliano kwa gharama nafuu.
“Kama
ilivyo kauli mbiu yetu kuwa “Ukiwa na Vodacom maisha ni
murua”tunahakikisha mbali na kutoa huduma bora
kwa wateja wetu pia tunajua kuwa kuna muda wanahitaji kufurahi kwa
burudani hivyo ndio maana tunaandaa na kudhamini matamasha ya aina hii
na tutaendelea kufanya hivyo siku zote ikiwa ni moja ya njia ya kusema
ahsante kwa wateja wetu kwa kutuunga mkono”Alisema.
Alisema
mwaka huu burudani kupitia matamasha haya imekuwa jijini Dar es salaam
wakati mikakati inafanyika kuhakikisha
burudani hii inasambazwa kwa wateja wote nchi nzima “Tunawajali na
kuwasikiliza wateja wetu ambao kwetu ni wafalme hivyo tutahakikisha
huduma bora na burudani katika kipindi maalum kama hiki inawafikia
katika siku za usoni”.Alisema Nkurlu.
No comments:
Post a Comment