MKUU wa Mkoa wa Arusha Felix Ntibenda ameipongeza taasisi inayotoa huduma za kifedha (FINCA) kwa kufauata kuwafutia zaidi ya milioni 30 wanachama 35 wajasiliamali wa soko la MT meru curios &crafts market wanaojishughulisha na uzaji wa bidhaa za vijago jijini walizo kopa kwa ajili ya kufanya biashara kabla ya kunguliwa na soko hilo mapema mwezi uliopita.
Ntibenda amesema hayo leo, wakati akikabidhi hundi ya shilingi milioni 17na laki tano kwa wajasiliamali hao mbele ya waandishi wa habari iliyofanyika eneeo la soko hilo lililoko wilaya ya arusha mkoa wa arusha.
Kwa upande wa meneja taasisi hiyo Baraka Jekonea alisema kuwa lengo la kutoa msaada huo ni kuendeleza ujenzi wa soko hilo I benki hiyo in warudi katika hali yao ya zamahi ya biashara .
“Sisikama Taasisi ya Kifedha Finca tumeamua kuwasaidia ili tuweze kuwanusuru wahanga hawa kwa janga walilolipata tunaimani kwamba watarejea katika hali yao ya zamani kwani tangu wakumbane na changamoto hiyo maisha yao yamekuwa magumu sana”alisema Jekonea
Pia alitoa wito kwa wafanyabiashara ambao hawajajiunga na taasisi hiyo kufanya hivyo kwa kuwa benki hiyo inajali wajasiriamali na kuwataka kujiunga na taasisi ya mikopo ili kuweza kupata mikopo ya nafuu.
Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa soko hilo Hamis Juma alishukuru taasisi kwani pesa hiyo itawasaidia sana sana katika kujikwamua na kurejesha hali yao ya awali katika biashara yao.
Hata hivyo kabla ya msaada huo walijichangisha kiasi cha shilingili laki nane kwa kila muhanga nakufanikiwa kukusanya shilingi milioni mia mbili iliyowasaidi kuanza ujenzi wa soko hilo.
Aidha mwenyekiti huyo ameomba taasisi nyingine ili kuweza kuwasaidia kuwapatia mitaji ili kuweza kuanza upya tena biahsra hiyo ya uuzaji wa vinyago.
No comments:
Post a Comment