*Abiria watakiwa kutoa taarifa za madereva
wazembe
Ofisa wa Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani, Inspekta Notker Kilewa (kushoto), akielimisha abiria wa basi liendalo Morogoro wakati wa operesheni ya usalama barabarani iliyofanyika leo mkoani Pwani kwa kushirikiana na kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania, ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani ya “Wait to Send” inayohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanaendesha vyombo hivyo. Kulia anayeshuhudia ni Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu.
Dereva wa basi liendalo Morogoro, John Peter, akisoma kauli mbiu ya usalama barabarani ya mwaka 2014 katika fulana kabla ya kukabidhiwa fulana hiyo na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kulia) pamoja na stika yenye ujumbe unaohamasisha madereva kutokutumia simu zao za mkononi wakati wanaendesha magari ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani ya “Wait to Send” inayoendeshwa na kampuni hiyo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi katika zoezi lililofanyika leo katika mikoa ya Pwani na Morogoro. Wakishuhudia ni Meneja Uhusiano wa Nje wa kampuni hiyo, Abigail Ambweni (wa pili toka kulia) na Ofisa wa Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani, Inspekta Notker Kilewa.
Mkuu wa Kitengo Cha Elimu wa Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu, Abel Swai akisisitiza jambo kwa abiria wa basi liendalo Iringa wakati wa operesheni ya usalama barabarani iliyofanyika Mkoani Morogoro leo kwa kushirikiana na kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania, ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani ya “Wait to Send” inayohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanaendesha vyombo hivyo pamoja na kuwapima madereva kiwango cha pombe mwilini,Kampeni hiyo inadhamiwa na Vodacom Tanzania.
Ofisa wa Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama
Barabarani, PC Twaima Othman (kushoto), akimpima kiwango cha pombe mwilini
dereva wa basi la kwenda mikoani, Abdallah Omari (kulia) kwa
kutumia kifaa maalum wakati wa operesheni ya usalama barabarani iliyofanyika
Mkoani Pwani leo, ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya Usalama
Barabarani ya “Wait to Send” ya Vodacom Tanzania inayohamasisha madereva wa
vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanaendesha vyombo
hivyo. Katikati ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Abigail
Ambweni.
Na Mwandishi Wetu
Na Mwandishi Wetu
KAMPENI ya usalama barabarani ya kuwataka madereva nchini
kuzingatia sheria za usalama barabarani iliyozinduliwa hivi karibuni na Waziri wa
Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Mathias Chikawe leo, imeendelea katika Mkoa wa Pwani
na Morogoro.
Madereva wameendelea kuhimizwa kutotumia vinywaji vyenye ulevi na
kuacha tabia ya kuongea na simu au kutuma na kupokea ujumbe wa maneno (sms)
wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto.
Vilevile polisi wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Pwani
ambako ni barabara kuu inayotumiwa na magari mengi yaingiayo na yatokayo jijini
Dar es salaam walitoa elimu kwa abiria jinsi ya kutoa taarifa waonapo vitendo
vya madereva wanaondesha magari kwa uzembe na kuhatarisha maisha yao ambapo
walipatiwa namba maalumu za simu za kutoa taarifa za matukio hayo.
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani cha Jeshi la
Polisi mkoa wa Morogoro Boniface Mbao amesema kampeni hii ni muhimu katika
kupunguza matukio ya ajali “Watumiaji wa barabara hii ya mkoa wa pwani ni
wengi hususani madereva wa vyombo vya moto hawana budi kuzingatia maelekezo
ambayo tumekuwa tukiwapa katika kampeni hizi ili tupate matokeo mazuri kwa
kupunguza ajali kama ilivyokusudiwa”Alisema
Alisema madereva wakizingatia sheria za barabarani kwa kiasi
kikubwa ajali zinazoendelea kutokea kila siku zitapunga hususani katika kipindi
hiki cha msimu wa sikukuu ya mwaka mpya na aliipongeza kampuni ya
Vodacom kwa kuunga mkono jitihada za serikali katika kupambana na tatizo hili
ambalo limekuwa sugu .
Kwa upande wake,Mkuu wa Masoko wa Vodacom Tanzania kanda ya
Pwani Herieth Koka, alisema Vodacom
itaendelea kushirikiana na serikali kuunga mkono jitihada za
kuondoa matatizo kwenye jamii kama lilivyo tatizo hili la ajali ili
kuhakikisha wananchi wanaishi maisha murua na marefu.”Tunatoa rai kwa madereva
wote kuzingatia kauli mbiu ya Wiki ya Nenda Kwa Usalama barabarani isemayo”Maamuzi
yako barabarani ni hatma yetu-Fikiri kwanza".
Aliongeza kuwa Vodacom itakuwa mstari wa mbele kuelimisha
jamii athari za kuendesha gari wakati huo huo unatumia simu ya mkononi
kupitia kampeni ya "Wait
to Send" pia itaendelea kuhamasisha madereva kuzingatia sheria za
usalama barabarani.
Alisema kabla ya uzinduzi wa kampeni ya leo tayari
umefanyika uhamasishaji wa madereva kuzingatia sheria za barabarani katika miji
ya Dar es Salaam,Mwanza,Arusha,Mbeya na kampeni hizi zitaendelea kufanyika
sehemu mbalimbali nchini.
Katika kampeni ya leo wafanyakazi wa Vodacom kwa kushirikiana na
askari wa usalama barabarani na wajumbe wa Baraza la Taifa la
Usalama Barabani walitoa uhamasishaji kwa madereva kuacha kuongea na simu
wanapoendesha vyombo vya moto na kuwagawia madereva pete maalum za kuwatahadharisha
kutotuma ujumbe wa simu za mkononi wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto pia
zoezi la kupima madereva kubaini kama wanatumia vilevi lilifanyika ambapo
wadereva waliokutwa wanaendeshwa vyombo vya moto walichukuliwa hatua kali za
kisheria.
Baadhi ya abiria walioshuhudia kampeni hii mkoani Pwani wamesema
ni ya muhimu itasaidia kupunguza ajali nchini.”Hivi sasa ajali nyingi
zinazotokea hapa nchini zinasababishwa na uzembe wa madereva,kampeni hizi
zikiendelea zitapunguza ajali kwa kiasi kikubwa”.Alisema Bi Khalfan mkazi wa
Morogoro aliyekuwa safarini akitokea Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment