Msemaji wa Wizara ya Kazi na Ajira Bw. Ridhiwani
Wema akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mikakati ya
Serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya waajiri kuongeza fursa za ajira
hapa nchini.kushoto ni Afisa Kazi Mkuu Bi Amina
Likungwala. (Picha zote na Frank Mvungi)
Na Frank
Mvungi, Maelezo
Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kuimarisha mazingira ya
uzalishaji ajira katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita ambapo ajira 139,361
zimezalishwa.
Hayo
yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara ya kazi na Ajira Bw.
Ridhiwani Wema wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
katika Mkutano huo Wema alisema kuwa kati ya ajira zilizozalishwa 3,657 ni
ajira za Serikalini na 135,704 ni ajira kupitia sekta binafsi.
Kwa
mwaka 2013/2014 ajira 408,756 zilizalishwa na mwaka 2014/15 jumla ya ajira
560,000 zilitarajiwa kuzalishwa katika sekta binafsi rasmi.
Akifafanua
zaidi Wema amesema, kwa kipindi cha mwaka 2011/12 ajira zilizolalishwa ni
250,678 ambapo mwaka 2012/2013 zilizalishwa ajira 274,030.
Aidha
katika kipindi cha mwaka 2013/14 sekta binafsi rasmi imezalisha ajira 408,706
kupitia uwekezaji binafsi ambapo baadhi ya maeneo hayo ni Viwanda vidogo na
kati ,Uwekezaji kupitia TIC,Sekta ya Mawasiliano na nyingine.
Marekebisho
mengine yanayofanyika yanahusisha sheria ya Taasisi za Kazi na Ajira Na.7 ya
mwaka 2004 pamoja na kutunga sheria mpya ya ajira za wageni Nchini ambayo
imelenga kulinga ajira za watanzania,kuboresha mazingira ya Biashara na
kuhamasisha uwekezaji.
Takwimu
hizi zinaonyesha kuwa sekta binafsi itafanya vizuri zaidi kwa kuwa Serikali
imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa waajiri ili waweze kuongeza fursa za ajira hapa nchini ambapo baadhi ya
hatua zinazochukuliwa kwa sasa ni pamoja na kufanya marekebisho ya Sera ya
Ajira ya mwaka 2008,Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini No. 6 ya mwaka 2004.
|
No comments:
Post a Comment