TANGAZO


Tuesday, November 4, 2014

Rais Dk. Ali Mohamed Shein afungua Kongamano la kusherehekea miaka 4 ya ushindi wake na CCM

Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), walioshiriki katika Kongamano maalum kwa ajili ya kusherehekea miaka minne ya ushindi wa Dk. Ali Mohamed Shein, kuchaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baaraza la Mapinduzi, wakimsikiliza Makamo huyo, Mwenyekiti wa CCM alipokuwa akizungumza katika ufunguzi wa Kongamano hilo, lililofanyika katika ukumbi wa Grand Palace Mjini Zanzibar. (Picha zote na Ikulu)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, akizungumza na wananchi pamoja na wanachama katika Kongamano maalum la maadhimisho ya sherehe za miaka minne ya Ushindi wa CCM na kuchaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Grand Palace Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, akizungumza na wananchi pamoja na wanachama wa chama hicho katika Kongamano maalum la maadhimisho ya sherehe za miaka minne ya Ushindi wa CCM na kuchaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Grand Palace, Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, akizungumza na wananchi pamoja na wanachama wa chama hicho katika Kongamano maalum la maadhimisho ya sherehe za miaka minne ya Ushindi wa CCM na kuchaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Grand Palace, Mjini Zanzibar.
Baadhi ya wanachama wa CCM walioshiriki katika Kongamano maalum kwa ajili ya kusherehekea miaka minne ya ushindi wa Dk. Ali Mohamed Shein kuchaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baaraza la Mapinduzi, wakimsikiliza Makamo huyo, Mwenyekiti wa CCM alipokuwa akizungumza katika ufunguzi wa Kongamano hilo, lililofanyika katika ukumbi wa Grand Palace Mjini Zanzibar.
Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akiagana na baadhi ya viongozi wa Chama baada ya kulifungua Kongamano la CCM katika kusherehekea miaka minne ya ushindi wa chama hicho, pamoja na Dk. Ali Mohamed Shein kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, lililofanyika katika ukumbi wa Grand Palace Mjini Zanzibar.
Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akiagana na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Balozi Seif Ali Iddi katika Hoteli ya Grand Palace Mjini Zanzibar, mara baada ya kulifungua Kongamano la CCM katika kusherehekea miaka minne ya ushindi wa chama hicho na Dk. Ali Mohamed Shein kuwa Rais wa Zanzibar na MBLM.
Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akiagana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai katika  Hoteli ya Grand Palace, Mjini Zanzibar baada ya kulifungua Kongamano la CCM katika kusherehekea miaka minne ya ushindi wake na Dk. Ali Mohamed Shein kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Said Ameir, Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amewataka wana CCM kutangaza mafanikio ya utekelezaji wa Ilani yake katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake huku akiwahakikishia kuwa chama hicho kitashinda kwa kishindo uchaguzi mkuu ujao.
“Wana CCM twendeni tukayaseme tuliyoyafanya ...twendeni tukawaeleze wananchi namna tulivyotekeleza Ilani yetu” Alisema Dk. Shein huku akisisitiza kuwa Ilani ya chama hicho imetekelezwa kwa mafanikio makubwa katika kipindi hicho na serikali anayoingoza.
Dk. Shein amesema hayo leo katika hotuba yake ya uzinduzi wa Kongamano Maalum la kuadhimisha miaka minne ya Ushindi wa CCM na uongozi wake liliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Grand Palace mjini hapa.
Katika kongamano hilo lililojumisha washirikia zaidi ya 180 wakiwemo viongozi wa chama hicho na jumuiya zake kutoka wilaya 8 za chama hicho katika kisiwa cha Unguja, pamoja na viongozi wa Makao makuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar, Dk. Shein ambaye pia, ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar alieleza mafanikio mbalimbali ya Serikali katika kipindi hicho cha miaka mine.
Baadhi ya mafaniki hayo ni kuinua kiwango cha ukuaji wa uchumi kutoka asilimia 6.7 mwaka 2007/2008 hadi asilimia 7.5 mwaka 2013/2014, kuongezeka kwa mapato ya serikali ambapo ukusanyaji wake umeongezeka kutoka wastani wa Tshs bilioni 13.3 kwa mwezi kwa mwaka 2010 alipoingia madarakani hadi wastani wa Tshs bilioni 34 kwa mwezi mwaka 2013.
Alisema kutokana na kuongezeka kwa mapato ya serikali, mishahara ya watumishi wa Serikali imeweza kuongezwa mara mbili ndani ya kipindi cha miaka mitatu kitu ambacho ni historia kwa Zanzibar. Alieleza pia mafanikio yaliyopatikana katika sekta za elimu, afya, miundombinu na uwekezaji hususan sekta ya utalii.
Aliongeza kuwa Chama cha Mapinduzi kiko tayari kutathminiwa na wananchi na kujibu maswali na hoja zao kwa ufasaha, utulivu na kwa lugha nzuri kwa kuwa kina majibu ya hoja zao kuhusu utekelezaji wa Ilani yake.
“Hatujafanya mahesabu ya asilimia ngapi hadi sasa tumetekeleza Ilani yetu lakini hivi karibuni tutafanya hivyo. Hata  hivyo ninawahakikishia kuwa tuko mbali sana na kwa sababu muda bado tunao tutaendelea kuitekeleza” alisema.
Kwa hivyo alibainisha kuwa CCM“ inajiamini na inaaminiwa na wananchi kwa hivyo wataendelea kukichagua”
Makamu Mwenyekiti huyo wa CCM aliwaeleza washiriki wa kongamano hilo kuwa utekelezaji wa Ilani ya CCM umefanywa na Serikali nzima anayoingoza ambayo imo katika mfumo wa Umoja wa Kitaifa.
“Mara baada ya CCM kushinda na mimi kuapishwa wa Rais niliunda serikali kwa kufuata misingi ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa nikishirikisha wa mawaziri kutoka chama changu na chama kilichoshika nafasi ya pili” alisema.
Alifafanua kuwa baada ya kuzindua Baraza la Wawakilishi ambapo alieleza mipango na programu za utekelezaji wa Ilani ya CCM aliunda Baraza la Mawaziri pamoja na taasisi nyingine kukidhi mahitaji wa utekelezaji wa Ilani hiyo.
“Tuliunda Wizara, taasisi pamoja na kupitisha sheria ili tuweze kutekeleza Ilani yetu  na ndio matokeo tunayoyaona leo” alifafanua na kuongeza kuwa katika kutekeleza majukumu yake amekuwa akitekeleza ipasavyo misingi ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa mujibu wa Katiba.   
Dk. Shein alikiri kuwa  awali wako waliokuwa na wasiwasi kuhusu kufanikiwa kwa serikali hiyo Zanzibar lakini yeye na chama chake kilikuwa na hakika kitafanikiwa kuongoza na kupata matokeo mazuri kamam ilivyodhihiri.
Kuhusu Katiba iliyopendekezwa aliwaeleza washiriki wa Kongamano hilo kuwa Katiba hiyo imejibu hoja zote ambazo zilikuwa zikiitwa kero za muungano pamoja na malalamiko mengine likiwemo la madai kuwa Tanganyika imevaa ‘koti la muungano’.
Alieleza kuwa tangu yeye na Rais Jakaya Kikwete walipokabidhiwa Katiba iliyopendekezwa kumekuwepo na wasemaji wengi wanaoipinga Katiba hiyo na miongoni mwao wakijenga dhana kuwa wanaposema wao wengine hawana fursa tena ya kufanya hivyo.
Kwa hivyo alitahadharisha tabia hiyo inayojengwa na baadhi ya wasemaji hao ambao wengine ni viongozi kutumia fursa ya Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba kukashifu viongozi wenzao na hata kuwatisha wengine kitendo kinachohatarisha amani na utulivu nchini.
"Wako wanaodhani wanalosema wao ndilo la mwisho na wengine hutumia lugha za matusi na hawa baadhi yao ni viongozi na tulikwisha kukubaliana tuache lugha za matusi katika majukwa ya siasa,” alikumbusha Dk. Shein na kutahadharisha kuwa ikilazimu atachukua “hatua kwa mujibu wa Katiba na Sheria zinavyoelekeza”.
Alisisitiza kuwa Katiba iliyopendekezwa itapigiwa kura na wananchi wote wa Zanzibar na anaamini kuwa wananchi hao wataikubali kwa kuwa wanafahamu historia ya nchi yao.
“wananchi wanaelewa walikotoka... wazazi wao walifanya nini; walifanya Mapinduzi na kuunda Muungano hivyo kamwe hawatakubali yatokee mengine kinyume na hayo” alisema Dk. Shein na kuwakumbusha wanaopinga Katiba iliyopendekezwa kuwa wasidhani kuwa watapiga kura peke yao.
Katika hotuba yake hiyo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi alisisitiza kuwa watu wanaodai Zanzibar ipatiwe mamlaka kamili hawajui wanachokitaka kwa kuwa Zanzibar inatambulika ulimwenguni kote kuwa ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na imekuwa ikipewa heshima yake.
“Nawashangaa wanaotaka Zanzibar ya mamlaka kamili...Zanzibar inayo mamlaka yake kwa kuwa ina utambulisho wake, ina mihimili mitatu ya dola na inapewa heshima yake kote ulimwenguni” Dk. Shein alisisitiza.
Alibainisha  kuwa wananchi wa Zanzibar hawawezi kuvunja muungano kwa kuwa wanaelewa kuwa kulinda Muungano ndio kulinda Mapinduzi ya mwaka 1964 na kuwaonya wenye mawazo tofauti kuwa hilo halitotokea kamwe.  
Katika kongamano hilo mada mbili ziliwasilishwa ambapo Mjumbe wa Kamati ya CCM Dk. Mohamed Sief Khatib alitoa mada inayohusu Maudhui ya Katiba Inayopendekzwa na Mustakbali wa Zanzibar na Naibu Waziri wa Wizara ya  Miundombinu na Mawasiliano Issa Haji Ussi alitoa mada kuhusu Mafanikio ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa 210-2015

No comments:

Post a Comment