TANGAZO


Monday, November 10, 2014

Naibu Mwanasheria wa Serikali afungua mafunzo ya haki za binadamu Hoteli ya Kunduchi jijini Dar es Salaam

Baadhi ya washiriki wa warsha ya siku tano ya mafunzo kuhusu masuala ya haki za binadamu wakifuatilia hotuba ya Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju (hayupo pichani), iliyotolewa leo Kunduchi Beach Resort. Mafunzo hayo yameandaliwa na Umoja wa Taasisi za Kitaifa za Haki za Binadamu Afrika (NANHRI) kwa kushirikiana na Taasisi ya mafunzo ya haki za binadamu na Sheria za ki-utu ya Raoul Wallenberg (RWI) ya Sweden na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG)
kwa ufadhili wa SIDA.
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju akitoa hotuba yake kufungua rasmi warsha ya siku tano ya mafunzo ya haki za binadamu kwa maafisa kutoka Taasisi 11 za kitaifa za haki za binadamu za nchi za Afrika Kunduchi Beach Resort mapema leo. 
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju akitoa hotuba yake kufungua rasmi warsha ya siku tano ya mafunzo ya haki za binadamu kwa maafisa kutoka Taasisi 11 za kitaifa za haki za binadamu za nchi za Afrika Kunduchi Beach Resort mapema leo.
Washiriki wa warsha ya siku tano ya mafunzo ya masuala ya haki za binadamu wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju
(waliokaa, wa pili kutoka kushoto) muda mfupi baada ya kufungua rasmi warsha hiyo Kunduchi Beach Resort mapema leo.
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Taasisi ya mafunzo ya haki za binadamu na Sheria za ki-utu ya Raoul Wallenberg (RWI) ya Sweden, Ms. Janne Holck Clausen (katikati) na Mratibu wa Umoja wa Taasisi za Kitaifa za Haki za Binadamu Afrika (NANHRI), Ms. Flavia Mwangovya muda mfupi baada ya ufunguzi rasmi wa warsha ya mafunzo ya siku tano kwa taasisi za kitaifa za haki za binadamu Afrika huko Kunduchi Beach Resort leo. (Picha zote na GERMANUS Joseph (0784 32 99 00), Afisa Habari - Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora)

No comments:

Post a Comment