TANGAZO


Sunday, November 2, 2014

Matukio ya vurugu katika mdahalo uliotayarishwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Ubungo Plaza, Dar es Salaam kuhusu Katiba Inayopendekezwa

Viongozi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku (kushoto) na Jaji mstaafu Joseph Warioba, wakijadili jambo wakati wa mdahalo kuhusu umuhimu wa kuielewa kwa kina Katiba Inayopendekezwa, kama ilivyopitishwa na Bunge Maalumu la Katiba, ulioandaliwa na taasisi hiyo Ubungo Plaza, Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Baadhi ya wananchi waliohudhuria mdahalo, wakinyanyua mabango yaliyokuwa na ujumbe mbalimbali, wakati aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, akizungumza kwenye mdahalo huo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, akizungumza katika mdahalo huo.
Wananchi waliohudhuria mdahalo huo, wakimtuliza kijana aliyepata kipigo, baada ya kutokea kutoelewana.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria mdahalo, wakipiga  makofi baada ya kufurahishwa na mada iliyokuwa ikitolewa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba.
Wananchi wakisikiliza mada zilizokuwa zikitolewa katika mdahalo huo.
 Baadhi ya wajumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, wakiwa katika mdahalo huo.

 Wananchi wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa katika mdahalo huo.
 Joseph Butiku, akiwasilisha mada katika mdahalo huo.



 Warioba akizungumza katika mdahalo huo.
 Mabango yakinyanyuliwa katika mdahalo huo, suala lililosababisha vurugu.
 Viti vilitumika kushambuliana kwa wale waliotofautiana katika misimamo.
 Kijana akipaza sauti huku akiwa amenyanyua bango lake.
Viti vikiwa kimedondoshwa baada ya kutokea vurugu hiyo katika mdahalo huo.

No comments:

Post a Comment