Mwenyekiti wa WOMESA kutoka Mauritius Bi. Meenaksi Bhirugnath-Bhookun neno wakati wa kufunga mkutano wa mwaka wa Umoja wanawake walio katika Sekta ya masuala ya Bahari Mashariki na Kusini mwa Afrika uliomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Mambo ya Bahari (IMO) Pamela Tansey akiwaasa wajumbe wa Umoja Wanawake walio katika Sekta ya masuala ya Bahari Mashariki na Kusini mwa Afrika (WOMESA) wakati wa kufunga mkutano wa sita wa mwaka wa umoja huo uliomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah Kairuki (kushoto), akimkabidhi cheti Mkurugenzi Msaidizi kutoka Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Mambo ya Bahari (IMO) Pamela Tansey (kulia) katika hafla ya kufunga mkutano wa sita wa mwaka wa Umoja Wanawake walio katika Sekta ya masuala ya Bahari Mashariki na Kusini mwa Afrika (WOMESA) uliomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah Kairuki (kushoto), akimkabidhi cheti Mwenekiti Msaidizi WOMESA tawi la Tanzania Dkt. Tumain Gurumo ambaye pia ni Mhadhiri katika Chuo cha Ubaharia cha Dar es salaam (DMI) (kulia) wakati wa hafla ya kufunga mkutano wa sita wa mwaka wa Umoja Wanawake walio katika Sekta ya masuala ya Bahari Mashariki na Kusini mwa Afrika (WOMESA) uliomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wajumbe mkutano wa sita wa mwaka wa Umoja Wanawake walio katika Sekta ya masuala ya Bahari Mashariki na Kusini mwa Afrika (WOMESA) wakiwa katika mkutano huo uliomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe mkutano wa sita wa mwaka wa Umoja Wanawake walio katika Sekta ya masuala ya Bahari Mashariki na Kusini mwa Afrika (WOMESA) wakiwa katika mkutano huo uliomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe mkutano wa sita wa mwaka wa Umoja Wanawake walio katika Sekta ya masuala ya Bahari Mashariki na Kusini mwa Afrika (WOMESA) wakiwa katika mkutano huo uliomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa mkutano wa mwaka wa WOMESA wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Ramsmi Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah Kairuki (wa tano kutoka kulia waliokaa) ya mara baada ya kufunga wa mkutano huo.
(Picha na Eleuteri
Mangi –MAELEZO)
Na Eleuteri Mangi-
MAELEZO
WANAWAKE walio katika
Sekta ya masuala ya Bahari wameaswa kupanua wigo wa wanachama walio katika sekta
hiyo ili kuongeza ufanisi na tija katika kutekeleza majukumu yao.
Hayo yamesemwa na Naibu
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah Kairuki, alipokuwa akifunga mkutano wa
sita wa mwaka wa wa Umoja wanawake walio katika Sekta ya masuala ya Bahari Mashariki
na Kusini mwa Afrika (WOMESA) unaomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es
salaam.
Bi. Kairuki alisema
kuwa sekta hiyo katika nchi wanachama ni muhimu kulingana na unyeti wake licha
ya kukumbwa na changamoto ya kuwa na wataalamu wa kike wachache jambo ambalo
WOMESA imelitambua na wanalifanyia kazi kupitia mikutano na semina mbalimbali.
“Ni jukumu lenu WOMESA
kushirikiana kwa pamoja ili kuongeza idadi ya wataalamu katika sekta hii
mkianzia na wasichana waliopo shuleni na vyuo mbalimbali vya elimu” alisema Bi.
Kairuki.
Pamoja
na mkutano huo, Bi. Kairuki amewaambia wajumbe hao wa mkutano kuwa anaamini
wamepta na kuboresha ujuzi walionao kwa kuwa wameshirikishana na kubadilishana
uzoefu kutoka nchi wanachama wa WOMESA ambapo maarifa hayo yataendelea kuwaongezea
tija na ufanisi katika kutekeleza majukumu yao kama akina mama na watalaam
katika masuala ya bahari.
Akimkaribisha
Mgeni Rasmi, Mwenyekiti wa WOMESA kanda ya Afrika kutoka Mauritius Bi. Meenaksi
Bhirugnath-Bhookun amesema kuwa WOMESA inakabiliwa na changamoto ya kuwa na
wanawake wachache katika sekta ya bahari.
Aidha Bi. Meenaksi
amesema kuwa katika mkutano wao wa mwaka wamefikia makubaliano ya kuongeza wanachama
kupitia mamlaka za masuala ya bahari, Idara mbalimbali zinazohusu masuala ya bandari,
shule za sekondari na vyuo mbalimbali katika nchi wanachama.
Naye
Mwenekiti Msaidizi WOMESA tawi la Tanzania Dkt. Tumain Gurumo ambaye pia ni
Mhadhiri katika Chuo cha Ubaharia cha Dar es salaam (DMI) amesema kuwa sekta ya bahari inafursa nyingi amewaasa wazazi
wawaruhusu watoto wa kike kujiunga kwenye elimu ya bahari ambapo bado kuna
fursa nyingi ili waweze kuboresha maisha yao na taifa kwa ujumla.
Dkt.
Tumain amewato wasiwasi wazazi na watoto wa kike ambapo amesema kuwa teknolojia imekuwa na imepanua wigo wa
wanawake kwenye masuala ya bahari, hivyo wanawake wanaweza kama walivyo wanaume
katika sekta hiyo.
katika mkutano huo, WOMESA wamezindua mpango makakati wa miaka mitano unaoanza
mwaka 2014 hadi 2019 ikiwa ni mpango wa kuuimarisha umoja huo katika ngazi ya kitaifa
na kanda.
Mkutano wa sita wa WOMESA,
mwaka huu umeongozwa na kauli mbiu inayosema “Wanawake katika sekta ya bahari
baada ya 2014: Wakijenga jukwaa endelevu”.
Nchi zilizoshiriki mkutano
huo wa mwaka ni Tanzania, Kenya, Komoro, Mauritius,
Namibia na Visiwa vya Shelisheli.
Nchi nyingine ni wanachama
ambazo hazikushiriki mkutano wa mwaka huu kutokana na sababu mbalimbali ni Angola,
Sudani, Lesotho, Uganda, Somalia, Eritrea, Botswana, Rwanda, Madagaska, Afrika
Kusini, Msumbiji, Burundi, Malawi, Djibout, Zimbabwe, Ethiopia na Zambia.
No comments:
Post a Comment