TANGAZO


Sunday, November 2, 2014

Waziri Mkuu Mizengo Pinda afungua Maabara ya Afya jijini Dar es Salaam

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akijadiliana na mmoja wa viongozi wa Maabara ya Sekta ya Afya, Dkt. Linda Ezekiel baada ya kupewa maelezo kuhusu moja ya maeneo manne ya sekta ya Afya yanayopendekezwa kuingizwa katika mfumo maalum wa utekelezaji wa miradi wa BRN. Katikati ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid.
Sehemu ya viongozi wakifuatilia hotuba ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipokuwa akifunga maabara ya afya jijini Dar es Salaam jana (Ijumaa). Maabara hiyo iliyokaa kwa wiki sita ilikuwa ikijadili miradi ya sekta ya afya itakayoingizwa katika mfumo maalum wa utekelezaji wa miradi wa BRN.
Mtendaji Mkuu, Ofisi ya Rais-Usimamizi wa Utekelezaji wa Miradi (PDB) inayosimamia Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), Omari Issa akimpongeza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda mara baada ya Waziri Mkuu kutoa hotuba ya kufunga maabara ya wiki sita ya BRN iliyokuwa ikijadili miradi ya sekta ya Afya.
Sehemu ya washiriki wakifuatilia hotuba ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipokuwa akifunga maabara ya afya jijini Dar es Salaam jana (Ijumaa). Maabara hiyo iliyokaa kwa wiki sita ilikuwa ikijadili miradi ya sekta ya afya itakayoingizwa katika mfumo maalum wa utekelezaji wa miradi wa BRN.

No comments:

Post a Comment