TANGAZO


Monday, October 13, 2014

Marekani kutumia vituo vya Uturuki


Makombora ya kudungulia ndege Syria
Uturuki imekubali Marekani kutumia vituo vyake vya kijeshi katika kampeni ya kupambana dhidi ta wapiganaji wa Islamic State, amesema Susan Rice Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani.
Bi Rice amesema Marekani imepongeza mkataba mpya ambao unahusisha kutumia kituo cha kijeshi cha anga cha Incirlik kusini mwa Uturuki.
Marekani inaongoza mashambulio ya anga dhidi ya wapiganaji wa IS, ambao wametwaa maeneo mengi ya Iraq na Syria katika miezi ya karibuni.
Uturuki inashirikiana mpaka na nchi za Iraq na Syria, lakini mpaka sasa haijawa na mpango wake wa kufanya mashambulio ya ardhini.
Akizungumza na kituo cha utangazaji cha Marekani cha NBC , Bi Rice amesema Uturuki hivi karibuni imekubali kuiruhusu Marekani kutumia vituo vya kijeshi na maeneo ya Uturuki "kutoa mafunzo kwa majeshi ya upinzani ya Syria yenye msimamo wa kadiri" na "kushiriki katika shughuli za kijeshi ndani ya Iraq na Syria".
Shambulio katika mji wa Kobane mpakani mwa Syria na Uturuki
"Huu ni mkataba mpya, na tunaoupongeza sana", amesema Bi Rice.
Mashambulio ya IS yamewalazimisha wananchi wa Syria 200,000 kukimbilia nchini Uturuki. Katika siku za karibuni, wapiganaji wa IS wamesonga mbele na kuingia katikamji wa Syria wa Kobane, ambao una eneo linalopakana na Uturuki.
Wapiganaji, ambao wanadhibiti baadhi ya maeneo ya mji wa Kobane, wamekuwa wakiyashambulia maeneo mengine ya mji huo kwa makombora mazito lakini wanakabiliwa na upinzani mkali kutoka majeshi ya Wakurd katika mji huo.
Hakuna upande uliopata ushindi wa kueleweka, licha ya majeshi yanayoongozwa na Marekani kuwasaidia Wakurd.
Uturuki imekuwa ikisista kujihusisha kijeshi katika mgogoro huo, kiasi kwa sababu ina wasiwasi na kuyapa silaha majeshi ya Wakurd yanayopigana na wapiganaji wa IS. Uturuki imepigana vita vya muda mrefu vya wenyewe kwa wenyewe na raia wake wa Kikurd walio wachache nchini humo

No comments:

Post a Comment