TANGAZO


Saturday, October 4, 2014

Makamu wa Rais Dk. Bilal ahudhuria kongamano la Biashara la Kimataifa kwa nchi za Afrika jijini Dubai, Falme za Kiarabu

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. 

Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika majadiliano kuhusu 

utengamano wa Afrika na Fursa za biashara na Uwekezaji na 

Katibu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Richard Sezibera, 

wakati wakihojiwa na Mwandishi wa habari wa Kimataifa na 

Mkurugenzi wa Kampuni ya ‘Eddo Media’, Mark Eddo (kushoto).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. 

Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika majadiliano kuhusu 

utengamano wa Afrika na Fursa za biashara na Uwekezaji, na 

baadhi ya viongozi, Katibu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, 

Balozi Richard Sezibera (katika) na Waziri wa Mambo ya Nje na 

Ushirikiano wa Kimataifa wa Ghana, Hanna Tetteh, wakati 

wakihojiwa na Mwandishi wa habari wa Kimataifa na Mkurugenzi 

wa Kampuni ya ‘Eddo Media’, Mark Eddo (kushoto). 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. 

Mohammed Gharib Bilal (wa nne kutoka kulia) akijumuika na 

baadhi ya viongozi wakati alipohudhuria Mkutano wa GBF, uliofanyika kwenye Hoteli ya Atlantis jijini Dubai. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. 

Mohammed Gharib Bilal (wa nne kutoka kulia) akijumuika na 

baadhi ya viongozi wakati alipohudhuria Mkutano wa GBF, uliofanyika kwenye Hoteli ya Atlantis jijini Dubai. 
Baadhi ya Washiriki wa kongamano hilo kutoka Tanzania, 

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),  

Nehemiah Mchechu (wa tatu kutoka kulia), akijadiliana jambo na 

Prof. Ahmada Khatib kutoka Tume ya Utalii Zanzibar wakati 

walipohudhuria mkutano huo, uliofanyika katika Hoteli ya Atlantis 

nchini Dubai. (Picha zote na OMR)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. 

Mohammed Gharib Bilal (wapili kulia) akisalimiana na baadhi ya 

wageni pamoja na viongozi, alipohudhuria Mkutano wa GBF, uliofanyika kwenye Hoteli ya Atlantis jijini Dubai. 

Na Mwandishi wetu, Dubai
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Oktoba Mosi, 2014 ameiwakilisha Tanzania katika kongamano la pili la Kimataifa la Biashara kwa nchi za Afrika lililofanyika katika jiji la Dubai, Farme za Kiarabu. 

Kongamano hili limehudhuriwa na washiriki wapatao 800 kutoka nchi mbalimbali duniani na limelenga katika kukuza uwekezaji katika nchi za Farme za Kiarabu na kufungua fursa za kibiashara barani Afrika. Kongamano la kwanza la namna hii lilifanyika pia jijini hapa  mwaka jana na kushirikisha  washiriki wapatao 3000 kutoka nchi mbalimbali duniani. 

Baadhi ya Viongozi wa Afrika waliohudhuria kongamano hilo ni pamoja na Rais Paul Kagame wa Rwanda, Rais John Dramani Mahama wa Ghana na Rais Mulatu Teshone Watu wa Ethiopia.
 Viongozi hawa kwa nyakati tofauti walizungumzia umuhimu wa utengamano barani Afrika na wakaeleza kuwa hiyo ndiyo fimbo pekee ya kukuza uwekezaji wenye tija Afrika. 

Pia walizungumzia mabadiliko makubwa ya Afrika huku wakiwakumbusha wawekezaji na wafanyabiashara waliohudhuria kongamano hilo kuwa Afrika ya sasa siyo bara la giza na kwamba ni bara linalokuwa kimaendeleo kwa kasi huku likiwa na fursa ya kukuza maendeleo yake kwa haraka. 

No comments:

Post a Comment