TANGAZO


Saturday, October 4, 2014

SHIMIWI: Timu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo yatinga hatua ya 16 Bora

*Yaiondoa Tamisemi kwa mikwaju ya penalti 4-3
Wachezaji wa timu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakiomba dua kabla ya mchezo wa hatua ya mtoano katika mashindano ya SHIMIWI leo uwanja wa Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA).
Mtunza Hazina wa Shirikisho la Micezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) Bw. Brown Nyamtiga akiwaasa wachezaji wa timu za mpira wa miguu kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na  Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) leo kabla ya kuanza mechi dhidi ya timu hizo mchezo uliochezwa katika uwanja wa Chuo.  
Mashabiki wa timu ya  Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakishangilia ushindi wa timu yao baada ya kuifunga timu ya Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)  magoli 4-3 kwa njia ya mikwaju ya penati baada mchezo huo kuisha kwa suluhu ya kutokufungana.
Mashabiki wa timu ya  Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakishangilia ushindi wa timu yao baada ya kuifunga timu ya Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)  magoli 4-3 kwa njia ya mikwaju ya penati baada mchezo huo kuisha kwa suluhu ya kutokufungana.
Mwenyekiti wa timu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Magreth Mtaki (wa kwanza kushoto) akishangilia ushindi wa timu yake walioupata dhidi ya timu ya Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) katika mashindano ya SHIMIWI yanayoendelea mjini Morogoro.
Picha ya pamoja yaViongozi, wachezaji na mashabiki wa  timu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakifurahia ushindi wao dhidi ya timu ya Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) katika mashindano ya SHIMIWI yanayoendelea mjini Morogoro. (Picha zote na Eleuteri Mangi -MAELEZO)

(Na Eleuteri Mangi – MAELEZO)
04/10/2014
Timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imeibuka kidedea kwa kuifunga timu ya  Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa mikwaju ya penati 4 – 3.

Ushindi huo wa timu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo umetokana na kazi nzuri aliyoifanya mlinda mlango wao Ramadhani Mtenga ya kupangua penati ya kwanza kuelekezwa langoni mwake.
Ujasiri huo wa mlinda mlango ndio uliotoa hamasa kwa wachezaji na mashabiki wa Wizara ya Habari Vijana, Utamaduni na Michezo ya kupata ushindi katika mchezo huo.

Wachezaji waliyoipatia ushindi timu yao waliongozwa na Edward Boniphance aliyefunga penati ya kwanza, penati ya tatu ilifungwa na Mbozi Katala, ya nne alifunga Ahmed Salimu na penati iliyowahakikishia ushindi Habari ilifungwa na Carlos Mlinda ambaye pia ni Nahodha wa timu hiyo huku James Mapepele akikosa kufunga penati ya pili.

Ushindi huo umeifanya timu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na kuingia hatua ya timu 16 katika mashindano hayo ya SHIMIWI yanayotarajiwa kufikia kilele Oktoba 11 mwaka huu.
Kikosi kamili kilichoibwaga timu ya TAMISEMI kiliongozwa na Nahodha Carlos Mlinga na Mlinda mlango Ramadhani Mtenga.
Wachezaji wengine ni Erick Mfugale, Noel Kambona, Hashimu Yusufu, Mbozi Katala, Milinde Mahona, Maurus Ndenda, James Mapepele, Ahmedi Salimu na Edward Boniphance.

Wachezaji wa akiba katika kikosi cha timu ya Habari walikuwa Idrisa Michael, Ayubu Abdallah, Hussein Makame na Pasto Mwita.

Wakati benchi la ufundi liliongozwa na mwalimu Tunge Shem, Daktari wa timu Biondo Ngome pamoja na Mwenekiti wa timu ya Wizara hiyo Dkt. Magreth Mtaki.


Aidha, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imekuwa Wizara ya kwanza kupata ubingwa katika mashindano ya SHIMIWI katika mchezo wa kurusha tufe ambapo mchezaji Mohamedi Mkangara amekuwa mshindi wa kwanza kwa kurusha tufe kwa umbali wa mita 11.32 ambao hakuna mchezaji mwingine aliyefikia umbali huo katika mashindano hayo.  

No comments:

Post a Comment