TANGAZO


Sunday, October 5, 2014

Kafulila azungumza tena fedha za Escrow zinazodaiwa kuchukuliwa Benki kuu na Kampuni ya kufua Umeme wa IPTL

Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu msimamo wake juu ya madai ya ufisadi dhidi ya kampuni ya kufua umeme ya IPTL. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Muhambwe, Felix Mkosamali.
Kafulila akisisitiza jambo katika mkutano huo na wanahabari. (Picha na Habari zote na Dotto Mwaibale wa Habari za Jamii Blog)
Waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.

Dotto Mwaibale
MBUNGE wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR- Mageuzi) ametishia kuwa iwapo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), hazitatoa ripoti ya  ufisadi wa sh. bilioni 400, Bunge lijalo la Novemba halitakalika.
"Napenda kusisitiza kwamba  fedha za Escrow dola milioni 270 (zaidi ya sh. bilioni 400), zimetolewa kifisadi na ndiyo sababu kwa muda mrefu sasa umekuwepo mkakati wa kuzuia ripoti za uchunguzi zisijadiliwe Bunge lijalo.                                                
"Mwito wangu kwa Serikali endapo ripoti hii haitaletwa Bunge lijalo halitokali. Nitapeleka hoja ya kutokuwa na imani na Serikali,"alisema.
Kafulila ambaye pia Katibu Mwenezi wa chama hicho, alitoa kauli hiyo Dar es Salaam leo wakati akizungumza na wanahabari huku akisisitiza kuwa anataka Watanzania waelewe msimamo kuhusu ufisadi huo unavyoratibiwa na baadhi ya watu waliojitoa ufahamu kutetea wizi.
Alisema mkakati alio nao kwa sasa anawasiliana na mwanasheria kuona iwapo ni nani kati ya Rais ama Waziri Mkuu ambaye atamtolea tamko la kutokuwa na imani naye.
"Watanzania wafahamu kwamba nchi wahisani hadi sasa hazichangii bajeti zikisubiri utekelezaji wa ripoti ya PCCB na CAG kuhusu ufisadi huo hivyo ni lazima Serikali ichukue kwani heshima ya nchi inaporomoka na bajeti haitekelezeki," alisema. 

Akizungumzia madai ya uzembe wa Serikali Kafulila alibainisha kuwa tukio hilo Serikali inalijua fika lakini halitolei msukumo wa kutolewa ripoti hiyo ambayo ilifanyiwa kazi na muda mrefu umepita.
"Tusaidiane kuikabili Serikali iwajibike. Uwajibikaji umekufa nchi hii. Leseni ya Ikulu inatumika kufanya ujangili tunaona tu?.

"FBME Bank inatumika miaka 6 kufanya biashara haramu tunaona sawa tu? Maelfu ya watu wanapoteza maisha kwa ajali waziri wanapiga porojo tunatazama tu. Tusirihusu nchi iendeshwe kihuni namna. Tushirikiane kuanza kuchukua hatua kuwajibishana,"alisema.
Wakati huo huo, Kafulila akizungumzia kuhusu IPTL/Pap na alisema waache kupotosha umma wa Watanzania kuwa wasijadili masuala ya biashara ndani ya IPTL (Merchmar, Piperlink na PAP) kwani mauziano hayo yana utata wenye maslahi ya taifa kwani yanaambatana na kodi (capital gain tax, kwa mujibu wa finance act 2012).

"Kwa mfano kitendo cha kuripoti kuwa asilimia 70 za hisa za IPTL ziliuzwa kwa sh. milioni 6 ina maanisha ukwepaji mkubwa wa kodi.
"Singasinga Seth hakununua IPTL bali alitumia fedha za Escrow alizopora kwa baraka waziri mkuu, Waziri wa Nishati na Madini, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Gavana wa Benki, Gavana wa Benki Kuu, Tanesco, Brela, TRA, kufanya asilimia 90 ya malipo ya ununuzi wa IPTL.

"Rejea barua ya Rugemalila aliyekuwa mmiliki wa VIP iliyopokelewa BoT Desemba 6 mwaka jana akikumbusha barua ya Novemba28, mwaka 2013 akisisitiza kuwa Singasinga Sethi sio mwaminifu na hakuwa amemlipa fedha kufikia Desemba 5 mwaka jana wakati alikuwa ameshachakachua fedha za escrow kuanzia Novemba 28 hadi Desemba 5 mwaka jana.
"Hii maana yake kuwa Sethi alitumia fedha za Escrow ambazo ni za umma kununua IPTL,"alisema.
Alidai kuwa Sethi ana rekodi ya kuhusika kwenye ufisadi wa goldenburg uliohusu zaidi ya sh. trilioni moja hyo ni kwa mujibu wa ripoti ya wikleaks ambayo hajawahi kukanusha mahali popote tangu kashifa hiyo iwekwe wazi.

No comments:

Post a Comment