Meneja Mawasiliano
wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Bw. Innocent Mungy akisisitiza jambo.
Na Benedict Liwenga, Maelezo-DSM
23/09/2014
Mitandao ya kijamii ni mizuri katika
kuhabarisha umma endapo inatumiwa kulingana na madhumuni iliyotengenezwa, kwani
ina nguvu ya kusambaza habari kwa haraka na kwa wakati hapa duniani.
Pamoja na umuhimu nwa mitandao hii ya
kijamii, kuna baadhi ya watu ambao wao hujiona kuwa wameendelea katika
ulimwengu wa kisayansi na teknolojia kiasi cha kuanza kuitumia mitandao hiyo
kinyume na malengo kwa kutumia kuiba taarifa mbalimbali za watu na hata usalama
wa maeneo muhimu ikiwemo benki, ofisini, mashuleni na sehemu kadha wa kadha.
Watu hawa kwa jina la kisayansi na
teknolojia hujulikana kama ‘Hackers’ au Wezi wa mitandao kwa kisawahili, na
wamekuwa wakivumbua mbinu mbalimbali kila kukicha ili kuweza kutimiza adhma yao
ya kuingilia mitandao mingi iliyopo duniani na wakati mwimngine wamekuwa
wakitumika katika shughuli za kigaidi ulimwenguni.
Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali toka
mitandaoni, kuna mbinu nyingi zitumiwazo na hackers hawa katika kuiba taarifa
mbalimbali kutoka kwenye takirishi (Computer)
hata simu za mkononi kwa njia ya mtandao (internet)
na njia hizi huwa zimekuwa zikiboreshwa kila kukicha.
Wezi wa mitandao wengi wamekuwa wakitumia visaidizi vya kompyuta (softwares) zijulikanazo kama Keyloggers ambazo ni hatari sana katika
kuiba taarifa toka sehemu yoyote endapo tu mmiliki wa kompyuta ataiacha kompyuta
yake kutumiwa na watu wasiofahamika ama katika ofisi mtu mharibifu ataingia na
kuingiza katika mfumo wa kuongozea kompyuta kisaidizi kama hiko, kutokana na
hilo software hizo hukusanya taarifa za mtu pasipo mtumiaji kujua
kinachoendelea na taarifa hizo hutumwa kwa njia ya barua pepe kwenda kwa
mharifu ambaye yeye anakuwa anazipata kadri atakavyo juu ya chochote
akifanyacho mtu, na moja ya sifa za software hizo ni kwamba hazionekani ndani
ya mfumo wa kuongozea kompyuta kirahisi.
Mbinu nyingine watumiazo watu hao ni kwa njia ijulikanayo
kwa kimombo kama ‘Phising’ ambapo
ukurasa unaofanana sawia na ukurasa halisi wa website hutengenezwa kwa
madhumuni thabiti ya kuiba nenosiri ama taarifa zozote kuhusiana na kitu
chochote, njia hii ni hatari pia ingawa haina tofauti sana na njia ile ya key logging kwani katika njia hii kazi
kubwa inayofanyika ni kuweko kwa kurasa feki ambayo inayofanana na kurasa
halisi ya website fulani.
Ili tuweze kujikinga na matukio haya ya wizi wa taarifa
kwa njia ya mtandao kuna mambo muhimu ya kuzingatia ambayo tunapaswa kuwanayo
makini wakati wote tunapozitumia kompyuta zetu.
Kwaza kabiasa, ili tuweze kujiepusha na njia itumiwayo na
hackers ijulikanayo kama Key-logging ni vema kuepuka kuazimisha kompyuta zetu
kwa watu tusiowajua ama kutumia mbinu ya kubofya kitufe cha Ctrl + shift + Alt + K vyote kwa pamoja
ili kuweza kujua uwepo wa kisaidizi kama hiko katika kompyuta na kama ikitokea
kimekuja kisanduku kinachokudai kuweka nenosiri basi ujue hapo kuna mtu anachunguza
taarifa zako katika kompyuta yako pasipo wewe kujua, hivyo chukua tahadhari kwa
kumtafuta mtaalam aweze kuondoa kisaidizi hiko.
Pia yatupasa kuhakikisha kuwa Windows Firewalls zilizopo ndani ya mifumo ya kuongozea kompyuta zetu ziko wazi wakati wote kwani firewall inasaidia kulinda takirishi yako dhidi ya wezi wa mitandao (hackers) ambao wanaweza kujaribu kuiharibu kwa lengo la kutaka kupata taarifa zilizomo ndani, kufuta taarifa, na hata kuiba baadhi ya neno siri za baadhi ya taarifa zako.
Ili kujikinga na wizi wa taarifa zetu
katika kompoyuta zetu, tunapaswa kuzingataia kuingiza ama ku-update Vizuizi
virusi (Antivirus) mara kwa mara
kwani vizuizi
hivyo vimetengenezwa kwa ajili ya
kuzuia virusi ama visaidizi kompyuta chokozi ili zisiweze kuiingia ndani ya
mfumo wa kompyuta na endapo ikitokea imegundua kirusi cha namna yoyote ile,
basi inafanya kazi ya kukiondoa ama kukifanya kisiweze kudhuru kompyuta wakati
wote.
Bila shaka lolote, Virusi vinaweza kuharibu mfumo wa kuongozea kompyuta
pasipo mtumiaji mwenyewe kujua licha ya baadhi ya vizuizi virusi kuwa na tabia
ya kuji-update vyenyewe.
Kuweka ama ku-update Antispyware Technology ni jambo linghne
la usalam dhidi ya hackers kwani Baadhi ya spyware huwa
na tabia ya kukusanya taarifa za mtu pasipo ridhaa yake kama ilivyo kwenye key-logging na Phising au huwa na tabia yakuweka matangazo yasiyo na ulazima
katika kurasa Fulani iliyopo katika mtandao wa kompyuta, sasa hii ni hatari kwa
usalama wa taarifa za mtu kwani hutumika pia kukwapua, hivyo hatunabudi kuwa
makini na baadhi ya matangazo yenye kututaka kupakua visaidizi fulani pasipo
malipo kwani mara nyingi huwa ni feki na wakati mwingine huwa na virusi vyenye
kuweza kutumika kuiba taarifa ndani ya takirishi yako.
Katika hali yoyote ile ni vema kwa watumaiji wa mitandao ya
kijamii kuepuka kutunza nenosiri katika kompyuta zao kwa lengo la kuondoa
usumbufu wakati wanapotaka kuingia tena katika kurasa zao kwani njia hiyo nayo
ni hatari kwasababu mtu anapoacha nenosiri lake liko (logged in) au unaposema (remember
me next time) unatengeneza njia rahisi kwa hacker kujua nenosiri lako kwa
kufanya kitendo kijulikanacho kama (Inspect
elements Q) yaani zile doti zinazowakilisha neno siri lako (******).
Katiko hilo, mhalifu anachokifanya hapo ni kuhailaiti hizo doti
(nyota) kisha anabofya katika kipanya upande wa kulia (right clicking) kisha anaenda mwisho katika sehemu iloandikwa (inspect elements Q) kisha
anafanya uhariri (editing) katika
kipengele kilichokuwa hailaitedi kwa rangi ya bluu kilichoandikwa neno ‘passoword’, hapo anafuta na kuandika
neno ‘TEXT’ kisha anabofya kitufe cha ‘Enter’
na akishamaliza kufanya hivyo nenosiri lenyewe linajibadilisha kwenda mfumo wa
maneno badala ya doti kama ilivyokuwa hapo mwanzo, hivyo humuwezesha kujua
tarakimu za nenosiri la akaunti yako ya mtandao wa kijamii uliocha wazi.
Njia nyingine ya jinsi ya kujikinga na
wizi wa kimtandao, tunahitaji kuwa makini na vitu tunavyopakuwa toka mitandaoni
hasa vibebaji (attachments) toka kwa
watu tusiowafahamu au wakati mwingine kwa watu tunaowajua kwani hata hao
hutumika katika kusaidia kuibwa kwa taarifa zetu kwa malengo yao binafsi.
Pia ni vema kuepuka kukubali marafiki tusiowajua
katika mitandao mingi ya kijamii ikiwemo facebook, twitter, Whatsapp, na
mingineyo kwani baadhi ya hackers wanatumia majina yasiyosahihi (fake names) kuomba urafiki kisha
hutumia mwanya huo pia katika kuiba taarifa zetu kiurahisi.
Kwa upande wa mabenki, ni vema kuachana
na mifumo ya kizamani ya kuongozea kompyuta iliyounganishwa na Mashine za
kutolea fedha maarufu kama (ATM) au Automatic Teller Machine kwa kimombo, kwani
hiyo ni hatarishi kwasababu mifumo ya kizamani, mfano Microsoft Windows XP ni mifumo ilikwishapitwa na wakati na hata
Kampuni yenyewe ya Microsoft imewataka watumiaji kuwa makini nayo kwani
haina-updates tena hali inayopelekea kuwa katika hatari ya kuvamiwa na wezi wa
mitandao kwa kutumia software za kisasa zenye uwezo wa hali ya juu katika kuiba
taarifa.
Katika
matumizi ya kadi zetu za kutolea fedha benki (ATM Cards) tunapaswa kuwa makini kuepuka kushea namba za siri kwa
marafiki au wapenzi na tujitahidi kuacha tabia ya kutumia nenosiri la kadi hizo
kama nenosiri katika akaunti za mitandao ya kijamii kwani hackers nao wamekuwa
watu wazuri wa kubashiri taarifa pindi wanapomlenga mtu.
Ili
kujiweka salama dhidi ya wezi wa mitandao, basi tujitahidi kutoa taarifa zozote
za kiusalama kwa vyombo vya usalama yaani Polisi au kupeleka malalamiko kwa
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) pindi tunapoona taarifa za uvunjwaji wa
sheria za matumizi ya mitandao, mfano mtu akiona kuna hitilafu katika taarifa
za muamala wa fedha zake katika akaunti yake ya benki fulani basi atoe taarifa
kwa benki husika ili wao waweze kutafuta tatizo na kutoa ufumbuzi.
Pamoja
na haya yote Watanzania wamehimizwa kuacha matumizi mabaya ya mitandao ya jamii
ikiwemo kuweka picha za utupu, kusababisha ugomvi, kuwahimiza wengine kwa mambo
yasiyo ya kweli, kupotosha jamii na kuvuruga maendeleo.
Akitoa
rai hiyo Meneja mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Bwana
Innocent Mungy alisema kuwa kuna ongezeko la matumizi ya intanenti kwa
watanzania hasa mitandao ya kijamii ambayo ni facebook, twiter, Instagram, BBM,
LinkedIn na Blogs mbalimbali kwa mambo yasiyofaa na kuleta athari kwa jamii.
Alisema
matukio yanayofanyika katika mitandao hiyo na kuleta athari ni utapeli,
kulipiza kisasi na ugomvi unaoanzia mitandaoni na kuendelea hadi kwenye
uhalisia.
“Kuna
utapeli wa kutumia huduma za mawasiliano na ugomvi wa makundi yakugombana
kupitia mitandao kwa majina kama timu fulani na timu fulani inayosababisha kuvunjika
kwa amani na kusababisha matusi pande zote,” alisema Mungy.
Mungy
aliongeza kuwa ni kosa la jinai kutumia mawasiliano vibaya kama ilivyoainishwa
katika sheria ya mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010 na
kutaka mawasiliano yatumike vizuri kudumisha amani ya Tanzania.
“Mamlaka
inapenda kuukumbusha umma kuwa ni kosa la jinai kuuza laini ya simu iwapo siyo
wakala au mtoa huduma, kutumia simu isiyosajiliwa, kutumia njia yeyote ya
mawasiliano kuvuruga amani na kumsaidia mtu mwingine atende kosa,” alisema.
Kwa
mujibu wa Mungy ni kosa la jinai kuweka picha za marehemu, mtoto na
zinazoonesha utupu katika mitandao ya kijamii huku akibainisha kwamba faini ya
kosa hilo ni shilingi za Kitanzania 750,000 na kifungo cha miezi mitatu
gerezani.
Kutokana
na haya, lazima tutambue kuwa mitandao ya kijamii si dhambi wala si vibaya
kuitumia, kwani haijatengenezwa kwa madhumuni ya kumkomoa fulani ama kwa lengo
la kuelimisha watu juu ya namna ya kuiba taarifa za watu wengine, bali
inetengenezwa ka madhumuni ya kuwakutanisha watu wa sehemu mbalimbali duniani
kuweza kuhabarishana juu ya mambo mbalimbali japokuwa baadhi ya watu hao
wamekuwa wakiitumia vibaya kinyume na maelngo ya uwepo wake.
No comments:
Post a Comment