Na Faki
Mjaka-Maelezo Zanzibar 17/08/2014
SHIRIKA la
Biashara la Taifa ZSTC limeandaa Programu ya Maonesho ya Sinema katika Vijiji
vya Unguja kwa lengo la kuwaelimisha wananchi juu ya uimarishaji wa zao la
Karafuu nchini.
Maonesho
hayo ambayo yatakuwa yakifanyika muda wa usiku katika vijiji mbali mbali
yatatoa fursa pia kwa Wananchi kuwauliza Maafisa wa ZSTC maswali yanayohusu kuimarisha
zao hilo la biashara nchini.
Akizungumza
leo katika maonesho hayo yaliyoanza huko katika kijiji cha Gamba, Mkoa wa Kaskaini
Unguja, Meneja Mawasiliano wa ZSTC Ally Mohamed Ally amesema Progaramu hiyo itasaidia
kuwajengea uelewa Wanachi na Ari ya kuendeleza Kilimo cha Zao la Karafuu katika
Vijiji vyao.
Amesema
Serikali ya Mapinduzi inachukua juhudi mbali mbali za kuliendeleza Zao la
Karafuu lakini baadhi ya wananchi wamekuwa hawafahamu juhudi hizo hivyo ZSTC wameamuwa kuwafuata vijijini kwao
ili kutoa elimu bora ya kilimo cha zao hilo.
“Serikali
inafanya juhudi kubwa sana za kuimarisha Zao la Karafuu lakini baadhi ya Wakulima
hawalifahamu hilo lakini kupitia maonesho haya tunaamini wananchi wengi
wataelewa na kuisaidia Serikali katika kuwaelimisha wenzao ili kwenda sambamba
na Sera ya Serikali ya kuliimarisha zao hilo” alisema Ally.
Kwa upande
wao Wanakiji wa Gamba wamelishukuru Shirika la ZSTC kwa kubuni njia hiyo ambayo
inaamsha hamasa na ari ya kushiriki katika kuliimarisha Zao hilo.
Akizungumza
mara baada ya Maonesho hayo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazalishaji Karafuu Jimbo
la Chaani Haji Khamis Faki ameliomba Shirika hilo kufanya Maonesho hayo na
Semina za mara kwa mara ili waweze kupata elimu zaidi.
Amesema kukosekana
kwa Elimu na hamasa ya mara kwa mara ndiko kunakopelekea wananchi kupuuza
upandaji wa Mikarafuu katika Vijiji hivyo.
Aidha
amelishauri Shirika la ZSTC kuzidisha mashirikiano na Wanavijiji hasa katika
ugawaji wa miche ya Mikarafuu ili iwafikie walengwa wanaostahiki kupata Miche
hiyo.
“Ukweli
unabaki kuwa hata hiyo miche ya Mikarafuu haitufikii sijui wanapelekewa nani
kwa hiyo tunaiomba Serikali kupitia Shirika wanapogawa Miche basi watafute njia
nzuri ya kumpatia kila mkulima anayestahiki kupata” Alisema Haji.
Kwa upande
wake Afisa Kilimo wa Wizara Badru Kombo Mwemvura amesema ushauri uliotolewa na
Wanakijiji hao wataufanyia kazi na kwamba Miche ya Mikarafuu itasambazwa na
kuwafikia wanakijiji hao kadiri itakavyowezekana.
Katika
Maonesho hayo Wananchi wa kijiji cha Gamba waliweza kujifunza kupitia maigizo
Umuhimu wa Zao la Karafuu nchini, Namna mzuri ya kuzianika na kuzitayarisha Karafuu
kwa ajili ya kuziuza.
No comments:
Post a Comment