Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia akifunga mafunzo
ya siku tano ya kuwajengea uwezo viongozi wa elimu ngazi ya mikoa katika
masuala ya usimamizi wa fedha za MMES II hivi karibuni katika chuo cha Wakala
wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) Bagamoyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia akiwaasa washiriki
wa mafunzo katika masuala ya usimamizi wa fedha za MMES II kutoka mikoa 16 nchini
ambao ndio watendaji wakuu katika usimamizi wa elimu, wamo Maafisa Elimu na
Afisa Mipango mkoa pamoja na Maafisa Elimu wilaya, Wahandisi na Waweka hazina
kutoka halmashauri za mikoa hiyo. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Ahmed
Kipozi.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya
kuwajengea uwezo viongozi wa elimu ngazi ya mikoa katika masuala ya usimamizi
wa fedha za MMES II wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia wakati wa kufunga mafunzo
hayo hivi karibuni katika chuo cha Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu
(ADEM) Bagamoyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia akiwa katika picha
ya pamoja na wawezeshaji wa mafunzo usimamizi wa fedha za MMES II kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, TAMISEMI
na chuo cha ADEM pamoja na baadhi ya wanasemina hivi karibuni Bagamoyo.
Na Eleuteri
Mangi-MAELEZO
SERIKALI itaendelea kutoa
mafunzo kwa watendaji wa Halmashauri na Mikoa juu ya usimamizi wa fedha, manunuzi
na takwimu katika masuala ya elimu nchini ili kuwajengea uwezo viongozi hao
katika masuala ya usimamizi wa fedha za Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya
Sekondari awamu ya pili (MMES II).
Kauli hiyo imetolewa mjini
Bagamoyo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia wakati akifunga mafunzo ya viongozi wa elimu
ngazi ya mikoa.
Ameongeza kuwa mafunzo
hayo yanalenga kuboresha ujuzi na utendaji kazi wao ili kukabiliana na
changamoto zilizopo.
Waziri Ghasia amewasihi
watendaji hao kuwa washirikiane katika kutekeleza majukumu yao ,kwani
lengo ni kufanya kazi kwa pamoja ambapo
kila mtu anafahamu majukumu yake na mipaka yake ili kufikia malengo
yaliyokusudiwa.
Katika hatua nyingine Waziri
Ghasia amesema kuwa kulingana na Sensa
ya watu na makazi ya mwaka 2012, jumla
ya watu milioni 14,796,537 ambao ni sawa
na asilimia 34 wa kuanza za shule za awali, msingi na sekondari zinazosimamiwa
na Mamlaka ya Serikali za Mitaa.
Amefafanua idadi hiyo
kuwa watu wa umri wa miaka 5 hadi 6 idadi yao ni 2,755,699 ambao ni sawa na
asilimia 6.32, miaka 7 hadi 13 idadi yao ni 8,341,701 ambao ni sawa na asilimia
19.12, miaka 14 hadi 17 idadi yao ni
3,699,137 ambao ni sawa na asilimia 8.48.
Ghasia ameongeza kuwa
taarifa hizo ni muhimu katika kuiwezesha Serikali kupanga mipango yote ya
kuwaendeleza watu hao katika nyanja zote.
Mafunzo hayo
yaliwashirikisha Maafisa Elimu na Afisa Mipango wa mkoa 16 pamoja na Maafisa
Elimu wilaya, Wahandisi, Waweka hazina pamoja na Maafisa Elimu Vifaa na Takwimu
kutoka halmashauri za mikoa hiyo.
Baadhi ya mikoa ambayo
watendaji wake walishiriki mafunzo hayo ni Dar es salaam, Pwani, Morogoro,
Singida, Kigoma, Manyara, Arusha, Mbeya, Kilimanjaro, Kigoma, Mwanza,
Shinyanga, Simiyu na Geita.
No comments:
Post a Comment