Baadhi ya waandishi wa habari wakiwasikiliza wawasilishaji toka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Frank Mvungi) |
Na Frank Mvungi
Serikali imejizatiti katika kutekeleza mpango wa
majaribio wa marekebisho ya tabia kwa watoto walio katika mkinzano na sheria na
walio katika hatari ya kukinzana na sheria katika jamii.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Afisa
Ustawi wa Jamii Mkuu toka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii bw. Steven Gumbo
wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
“Serikali
imefanikiwa kukamilisha kanuni za mahabusu za watoto, makao ya watoto na shule
ya maadilisho” alisema Gumbo.
Pia hatua nyingine ni kukamilika kwa miongozo ya
utoaji wa huduma katika mahabusu za watoto na shule ya maadilisho.
Hatua nyingine ni kuwepo kwa mwongozo wa kijamiii (CRP) wa Marekebisho ya tabia kwa watoto walio
katika mkinzano na sheria na walio katika hatari ya kukinzana na sheria.
Mafanikio mengine ni kuwajengea uwezo watumishi wote
wa mahabusi za watoto na shule ya maadilisho juu miongozo mbalimbali
iliyotolewa ya kuboresha huduma katika Taasisi hizo.
Akieleza zaidi Gumbo amesema kwa mujibu wa sheria ya mtoto,
wanaokinzana na sheria na ambao hawajapata dhamana kutoka katika mahakama wanapaswa
kupelekwa katika mahabusi za watoto, pale ambapo mahakama imejiridhisha kuwa
mtoto huyo ametenda kosa huamuru apelekwe katika shule ya maadilisho.
Wizara ya Afya kupitia idara ya Ustawi wa jamii
imekuwa ikishirikiana na wadau mblimbali kama vile Polisi, Mahakama, Magereza, Tume
ya Haki za Binadamu na Utawala Bora pamoja na mashirika mbalimbali ya Kitaifa na
Kimataifa katika kufanikisha na kutekeleza majukumu yake.
Watoto wanaokinzana na sheria wanatunzwa katika
mahabusi tano za watoto zilizopo katika mikoa ya Tanga, Arusha, Kilimanjaro,
Mbeya na Dar es salaam na katika shule ya maadilisho ya Irambo-Mbeya.
No comments:
Post a Comment