Hayo yamesemwa na Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Chakula
na Dawa nchini (TFDA) bi Gaudensia Simwanza wakati wa mkutano na waandishi wa
habari leo jijini Dar es salaam.
Akifafanua Gaudensia amesema TFDA imeandaa kanuni za
uongezaji virutubishi kwenye vyakula (Tanzania food, Drugs and Cosmetics (food
fortification) Regulations 2012)
Alisema kuwa hatua nyingine ni kuandaa miongozo ya
udhibiti wa ubora na usalama wa vyakula vilivyoongezwa virutubishi ili
kuwajengea uwezo wasindikaji kuweza kutekeleza matakwa ya kanuni za uongezaji
virutubishi kwenye vyakula.
Akifafanua Gaudensia
alisema kuwa upo mwongozo wa uhakiki wa
ubora na usalama katika usindikaji wa mafuta ya kula yaliyoongezwa virutubishi
na mwongozo wa uhakiki wa ubora na usalama katika usindikaji wa unga wa mahindi
ulioongezwa virutubishi ili kuliunda afya ya mlaji.
Katika hatua nyingine Gaudensia alibainisha kuwa
mwongozo wa usimamizi wa Kanuni za uongezaji virutubishi na mwongozo wa ukaguzi
wa vyakula vilivyoongezwa virutubishi ambapo pamoja na mambo mengine mwongozo
huu umeainisha taratibu za kufuata katika udhibiti wa vyakula vilivyoongezwa
virutubishi muhimu katika chakula.
Vilevile
alisisitiza kuwa utoaji wa mafunzo kwa wadau kuhusu uhakiki na udhibiti
wa ubora na usalama wa vyakula vilivyooongezwa virutubishi kama vile wataalamu
kutoka katika viwanda ni muhimu kwa vile vinavyoongeza virutubishi kwenye
vyakula.
Katika hatua nyingine, jukumu jinguine la TFDA ni kusambaza vitendea kazi
vinavyotumika katika uhakiki na udhibiti wa ubora na usalama wa vyakula na
kusimamia utekelezaji wa kanuni za uongezaji wa virutubisho kwenye vyakula.
No comments:
Post a Comment