TANGAZO


Thursday, June 5, 2014

Wasiwasi kuhusu hali nchini Somalia



Hali ya usalama bado ni mbaya Somalia licha ya Al Shabaab kuondoka Mogadishu

Maafisa wa serikali za Marekani na Jumuiya ya Ulaya wanafanya mkutano wa dharura na Rais wa Somalia, Hassan Mohamoud, kujadili hali ya usalama inayoendelea kuzorota nchini humo.
Viongozi hao pia watajadili hali ya kisiasa na kibinadamu.
Kutokana na sababu za kiusalama mkutano huo unafanyika ndani meli ya kivita iliyoko Bahari ya Hindi karibu na Ufuo wa mji Mkuu, Mogadishu.
Jumatano afisaa mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Maswala ya Kibinadamu, Valerie Amos, alitoa wito wa dharura wa Dola Milioni 60 zitakazotumiwa kuhakikisha kuwa Somalia hairejelei tena katika hali mbovu livyokuwa hapo awali.
Alisema wafadhili wa kimataifa kufikia sasa wametoa asilimia 19 pekee ya ahadi walizotoa.
Kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Boko Haramu lingali linaendelea na kampeni yake ya kushambulia wanajeshi wa Somalia na wale wa Umoja wa Afrika walio nchini humo.

No comments:

Post a Comment