TANGAZO


Tuesday, June 3, 2014

Waandishi wa habari waaswa kushirikiana na TMF kupunguza utegemezi wa matangazo

DSC_0540
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa mradi wa mafunzo ya bure kwa waandishi wa habari kwenye maeneo matano, ambayo ni katika Sekta ya uchimbaji, unyanyasaji wa kjinsia, kupamba na biashara ya madawa ya kulevya na kuzuia utumiaji wa madawa ya Kulevya kwa waandishi wa habari na utayarishaji na utengenezaji wa vipindi vya luninga na wanawake watangazaji jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma. Kushoto kwake ni Msaidizi wa Mwakilishi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Idadi ya watu, Dorothy Temu –Usiri na Mkurugenzi wa Mfuko wa vyombo vya habari, Ernest Sungura.

Na Damas Makangale, MOblog Tanzania
WAANDISHI WA HABARI nchini wamehimizwa kushirikiana kwa karibu na Mfuko wa Vyombo vya Habari (TMF) ili kuacha kutegemea zaidi matangazo kwa sababu kuna weka taaluma yao rehani.

Akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa mradi wa kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari jinsi ya kuripoti mambo ya sekta ya uchimbaji, unyanyasaji wa kijinsia, kupamba na biashara ya madawa ya kulevya na kuzuia utumiaji wa madawa ya Kulevya na watayarishaji wa vipindi vya luninga, Waziri wa kazi na Ajira, Mhe, Gaudensia Kabaka amesema kwamba vyombo vya habari lazima vishirikiane na mfuko huo ili kuwa huru wakati wa kuripoti.

“kuendelea kutengemea matangazo kutoka kwenye makampuni mbalimbali ili kujiendesha kuna wafanya kutokuwa huru katika uandishi wetu na tasnia ya habari kwa ujumla,” amesema Kabaka

Amesema mradi huo wa mafunzo ya bure kwa waandishi ni muhimu kwa taifa kwa sababu tatizo kubwa la ajira hasa kwa vijana na wanawake linachangia kwa kiasi kikubwa vijana wengi kujiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya.
DSC_0434
Baadhi ya wadau na wageni waalikwa wakimsikiliza mgeni rasmi hayupo pichani. Kabaka aliongeza kuwa mafunzo haya yatakayotolewa kwa ufadhili wa TMF ni muhimu ili kuelimisha jamii madhara ya kuuza na kusambaza dawa za kulevya na matumizi yake yanavyoathiri kizazi na kizazi.

“kwa sasa nchi yetu ya Tanzania ni moja ya nchi zilizoathirika sana na matumizi ya dawa za kulevya na mbaya zaidi kutumika katika njia ya kusambaza madawa hayo hatari,”
“kwa mujibu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii tuna jumla ya watu 20,626 walioathirika na dawa za kulevya na kwa sasa wanapatiwa matibabu,” alisisitiza Kabaka.

Amesema nchini matumizi ya dawa za kulevya kwa zaidi ni Bangi, Heroin, Mirungi na Cocaine na cha kutisha matumizi haya yanaathiri pia wanafunzi wa sekondari na shule za msingi nchini.
DSC_0515
Msaidizi wa Mwakilishi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Idadi ya watu(UNFPA), Dorothy Temu Usiri akitoa nasaha zake kwenye uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.

Kwa upande wake, Msaidizi wa Mwakilishi Mkazi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Idadi ya watu, Dorothy Temu-Usiri amesema kuwa kuongezeka kwa vitendo vya kikatili vya kijinsia na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi vimechochea kushirikiana na TMF kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari hapa nchini.

“kwa kuanzisha mafunzo haya ya bure kutasaidia waandishi wa habari kuandika kwa kina juu ya madhara ya matumizi ya dawa za kulevya ambazo ndio kichocheo cha ukatili wa kijinsia hasa kwa Wanawake,” amesema Usiri

Usiri aliongeza kwamba nchini Tanzania idadi kubwa ya watu wenye nguvu ya kufanya kazi ni vijana kwahiyo ni muhimu jamii ya kimataifa kushirikiana na serikali na taasisi zingine ili kunusuru kundi hili muhimu kwenye nchi.
DSC_0423
Mkurugenzi wa TMF nchini, Ernest Sungura akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo wa mafunzo ya bure yanayofadhiliwa na mfuko wake ambapo amesema kwamba malipo madogo kwa wahariri na waandishi wa habari kunadidimiza taaluma ya uandishi wa habari pamoja na swala la kutokubobea katika sekta husika (Specialization).
DSC_0490
Wadau watakaoshiriki kwa ukaribu kwenye mradi huo wakitambulishwa kwa mgeni rasmi kutoka kushoto ni Dkt. Pilly Said kutoka kitengo cha madawa ya kulevya hospitali ya Mwananyamala, January Nzisi Mkuu wa Kitengo cha Mtandao Tume ya Kudhibiti Madawa ya kulevya, Geodfrey Nzowa, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi, kitengo cha Kupambana na Madawa ya Kulevya, Bi. Aida Teshe Kaimu Kamishina kutoka Tume ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya (DCC) na Florence Bahati Khambi Afisa Habari kutoka Tume ya Kudhibiti dawa za kulevya.

FROM THE STATE HOUSE:PRESIDENT JAKAYA KIKWETE MEETS MELINDA GATES AND CANADIAN PRIME MINISTER


 President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete in conversation with Mrs. Melinda Gates who is the Co-Chair and Trustee of the Bill and Melinda Gates Foundation.

PICHA:BAADA YA MABASI KUZUIWA KITUO CHA MWENGE WAFANYA BIASHARA WADOGO WAPANGA KUANDAMANA KUPINGA KUWEKA MEZA ZAO ZA BIASHARA NDANI YA KITUO.


NSSF YAENDESHA KAMBI ZA UPIMAJI WA AFYA BURE KANDA YA ZIWA



Shirika la  Hifadhi ya Jamii (NSSF), limeendesha  kambi za upimaji wa Afya Bure kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Lengo la kambi hizi ni kuweza kutoa elimu na  kuwahamasisha wanachama wa NSSF na wananchi kwa ujumla waweze kujenga  tabia ya kupima afya zao mara kwa mara na kujiwekea mfumo bora wa maisha ili kuepukana na magonjwa sugu yasiyoambukiza.

Zoezi hili litaanzia mkoa wa Mara, Manispaa ya Musoma  kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Mkendo, kuanzia tarehe 28/05/2014,  kwa siku tatu mfululizo, kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi na moja Jioni.  Baadae, Kambi hizi zitaendelea katika mikoa ya Shinyanga , Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Geita na  Mkoa wa Kagera.

HUDUMA ZITAKAZOTOLEWA
Huduma mbalimbali zitatolewa bure kwenye kambi hizi zikiwemo;

Upimaji wa Shinikizo la damu
Upimaji wa sukari kwenye damu- Kisukari
Upimaji wa hali ya lishe (Uwiano wa Urefu kwa Unene)
Utoaji wa dawa za Minyoo Ushauri wa kitaalam kwa watakaokutwa na Matatizo Ushauri nasaha  na upimaji hiari wa VVU (UKIMWI) Kutoa vipeperushi vya Maelezo ya uboreshaji wa Afya.

Huduma  zote hizi zitatolewa na NSSF, BURE.

NSSF inaendelea kuwasii na kuwahimiza wakazi wa kanda ya ziwa kuwa waendelee kujiandikisha kwenye NSSF HIARI Scheme. NSSF HIARI Scheme ni kwa ajili ya wajasiriamali wadogo, wachimbaji wadogo, Ushirika wa Bodaboda , Ushirika wa Wakulima pamoja na wanachama wa Mifuko mingine ya hifadhi ya jamii.

Jiunge na NSSF HIARI Scheme ili uweze kujipatia mafao bora ya NSSF yakiwemo Bima ya Afya BURE kwa familia nzima (SHIB), mikopo nafuu ya SACCOS,  pamoja na Mafao bora mengineyo.

Wananchi wa kanda ya ziwa wanakumbushwa na kuhimizwa kujitokeza kwa wingi ili kupimwa na kupewa ushauri wa afya zao Bure.
NSSF INAJENGA MAISHA YAKO YA SASA NA YA BAADAE.
 Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Jackson Msome ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa Kambi ya Upimaji Afya Bure Mkoani Mara akifafanua jambo mara baada ya kutembelea banda NSSF ambapo zoezi la upimaji afya lilikuwa likiendeshwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF). Watu 1080 walipima maambukizi ya  virusi vya ukimwi na watu 2020 walipima magonjwa ya kawaida. Kulia ni Meneja wa Mafao ya Matibabu NSSF, Ali Mtulia.
Wakazi wa Mkoa wa Mara wakisubiri kumuona daktari kupata ushauri.
 Daktari wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Lucy Simbila (kulia), akimpima shinikizo la damu mmoja  ya  watu waliojitokeza  kupima afya mkoani Mara juzi, katika kambi ya Upimaji Afya Bure inayoendeshwa na NSSF katika mikoa ya Kanda ya Ziwa. 
 Wakazi wa Mkoa wa mara wakiwa kwenye foleni ya kuelekea kwenye vipimo wakati wa zoezi hilo.
 Wakazi wa Mkoa wa mara wakiwa kwenye foleni ya kuelekea kwenye vipimo wakati wa zoezi hilo.
 Baadhi ya watu waliojitokeza katika zoezi hilo wakiwa kwenye foleni kuelekea kwenye vipimo wakati wa zoezi hilo.
 Madaktari wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), wakimpa ushauri mmoja wa watu waliofika kupima afya.
Madaktari na Maofisa wa NSSF walioendesha kambi ya upimaji wa afya mkoani mara wakiwa katika picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment