TANGAZO


Monday, June 2, 2014

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana aunguruma Orkesument Simanjiro, kesho Mererani

Wananchi wa Kijiji cha Kitwai A, wakiwa wamenyoosha mikono juu, kwenye mkutano wa hadhara, wakati Katibu Mkuu wa CCM, ndugu Kinana alipokuwa akimuunga mkono jambo Mbunge wa jimbo la Simanjiro, Mhe. Christopher Ole Sendeka, katika suala zima la Utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Baadhi ya Wanahabari pichani kutoka kulia ni Mwinshehe kutoka gazeti la Jambo leo na Mary kutoka Gazeti la Nipashe wakiwa sambamba na wafuasi wa chama cha CCM, wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Kitwai A, wilayani Simanjiro mkoani Manyara.
Katibu Mkuu wa CCM, ndugu Abdulrahman Kinana akizindua gari la mradi wa Kukodisha la Kikunndi cha Vicoba Mkombozi chenye wanachama wapatao 30, mjini Orkesument, Wilayani Simanjiro mkoani Manayara.

Kinana ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, wako moani Manyara kwa ziara ya siku saba ya Kukagua kuhimiza na kusukuma miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Chama,kukagua maandalizi ya uchaguzi ya serikali za mitaa, kusikiliza kero za wananchi na kuzitafututia ufumbuzi.

Mbunge wa jimbo la Simanjiro, Mhe. Christopher Ole Sendeka, akiwahutubia baadhi ya  Wananchi wa Kijiji cha Kitwai A, akiwa ameambatana na msafar wa Katibu Mkuu wa CCM, ndugu Kinana, Katika kijiji hicho, ndugu Kinana alizindua Ofisi ya Mtendaji Kata ya CCM Kitwai A, na kuahidi kujenga shule ya Sekondari kwa ajili wananchi hao ambao hapo awali walikuwa na shule za msingi tu.
Katibu Mkuu wa CCM, ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo mafupi kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Simanjiro, Mhe. Ole Sendeka wakati akiangalia josho la ng'ombe la Orkirung'rung ambapo  kuna mradi wa ufugaji wa ng'ombe chotara ambao ni ufugaji wenye tija na unasaidia sana kuongeza thamani mifugo.
Mbunge wa Jimbo la Simanjiro, Mhe. Ole Sendeka akifafanua jambo Kwa Katibu Mkuu wa CCM, ndugu Kinana (hayupo pichani)  kuhuasiana na Mradi huo wa ufugaji wa ng'ombe wa kisasa (nyama na Maziwa), wakati akiangalia josho la ng'ombe la Orkirung'rung ambapo  kuna mradi wa ufugaji wa ng'ombe chotara,ufugaji wenye tija na unaosaidia kuongeza thamani mifugo.
Pichani mbele ye bango kulia ni jengo la Mama na Mtoto la kituo cha  Afya Orkesument, Wilayani Simanjiro, ambalo pia Katibu Mkuu wa CCM, ndugu Kinana alikagua.
Katibu Mkuu wa CCM, ndugu Kinana akimsikiliza Dkt. Juma Nahonyo wakati wa ukaguzi wa jengo litakalokuwa bohari ya Dawa katika kituo cha Afya cha Orkesument, kulia ni Mbunge wa jimbo la Simanjiro, Mhe. Christopher Ole Sendeka.
Katibu Mkuu wa CCM, ndugu Abdulrahman Kinana akizindua mradi wa Kikundi cha Mazingira kilichopo mjini Orkesument, Wilayani Simanjiro mkoani Manayara. Kikundi hicho kitatumika kueleimisha wananchi wa mji huo katika masuala ya usafi na kulinda mazingira, kuwaelimisha wananchi kuhusiana na mambo ya maambukizi ya UKIMWI,masuala ya Rushwa na mengineyo. 
Katibu Mkuu wa CCM, ndugu Kinana akiwahutubia wananchi wa Orkesument kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mjini humo wilayani Simanjiro, Kinana aliwaeleza wananchi hao kuwa ahadi za Rais zilizoahidiwa 2010 zitatekelezwa kwa zilivyoahidiwa kwa  wananchi  wa Simanjiro, pia aliwasisitizia wananchi hao kutochagua  viongozi wa vijiji wa hovyo ambao mwisho wa siku ndio wanaoleta mikorogo na migongano kwa wananchi kwa kuuza ardhi, hali inayoleta migogolo isiyokwisha kila siku.
Katibu Mkuu wa CCM, ndugu Kinana wakielekea kukagua jengo la Ofisi ya Mtendaji Kata ya CCM Kitwai A, wilayani Simanjiro.
Mbunge wa jimbo la Simanjiro, Mhe. Christopher Ole Sendeka akitetea jambo na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye katika kijiji cha Kitwai A, Simanjiro mkoani Manyara.
Mdau akifuatilia jambo, wakati wa mkutano huo.
Katibu Mkuu wa CCM, ndugu Kinana akipokelewa na Mwenyekiti CCM,  wilayani ya Simanjiro, ndugu Brown Ole Suya pamoja na Mbunge Mbunge  wa jimbo la Simanjiro, Mhe. Christopher Ole Sendeka.
Jengo la Ofisi ya Mtendaji Kata ya CCM Kitwai A, wilayani Simanjiro lililozinduliwa na Katibu Mkuu wa CCM, ndugu Kinana.

No comments:

Post a Comment