TANGAZO


Tuesday, June 3, 2014

Makamu wa Rais Dk. Bilal ateta na Rais mpya wa Malawi, Profesa Arthur Peter Mutharika

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa na Rais mpya wa Malawi Profesa Arthur Peter Mutharika wakiwa katika picha ya pamoja baada ya rais huyo mpya kukabidhiwa madaraka leo jijini Brantyre kwenye Hoteli ya Sunbird. Baada ya kukutana viongozi hao walipata fursa ya kuzungumzia masuala ya Kidiplomasia baina ya nchi mbili hizi na kukubaliana kuendelea kuwa na uhusiano mwema kama nchi zinazoishi ndugu na jirani. (Picha zote kwa hisani ya Ikulu ya Malawi)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Rais mpya wa Malawi Profesa Arthur Peter Mutharika wakiagana mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo baina yao na kuhusisha nchi zao kama nchi zinazoishi ndugu na jirani.

No comments:

Post a Comment