Wanaharakati nchini Syria
wanasema kuwa jeshi la serikali limetekeleza shambulizi la hewani katika
soko moja lilikoko katika sehemu inayothibitiwa na waasi Aleppo.
Shambulizi hilo la hewani lilitekelezwa Kaskazini mwa Syria wilayani Halak katika soko moja kuu.Watu thelathini wameripotiwa kuuawa katika soko hilo.
Picha na video za maiti zilizofunikwa na vifusi na majeruhi zimeonyeshwa katika mitandao ya kijamii.
Picha hizo zimeonyesha watu wakikimbia kwa taharuki katika barabara za mji huo.
Juzi mauaji ya wanafunzi kwa mabomu yaliripotiwa jijini Aleppo.
Wapiganaji waasi wameanza upya mashambulizi dhidi ya maeneo yanayodhibitiwa na serilaki ya Rais bashar al Asad.
Licha ya mapigano hayo yanayoendelea wanasiasa wanaowania kiti cha urais walikamilisha shughuli ya kuwasilisha vyeti vyao kwa tume ya uchaguzi.
Rais Bashar al Assad,anatarajiwa kushinda katika uchaguzi huo kwani upinzani unaonekana kukosa ufuasi mkubwa.
No comments:
Post a Comment