Maafisa nchini Colombia bado
wanajaribu kuwanusuru takriban watu thelathini waliofukiwa wakiwa hai na
mamia ya tani za tope pamoja na mawe baada ya mgodi haramu wa dhahabu
kuporomoka usiku wa Jumatano.
Miili mitatu imepatikana lakini maafisa wanasema
kuwa udongo uliolowa chepechepe katika eneo hilo umefanya juhudi za
uokoaji kuwa ngumu .Takriban mashine saba za kufukua udongo zimekuwa zikihusika katika shughuli ya uokoaji katika mgodi huo ulioko kusini magharibi mwa sehemu ya Cauca.
Kando kando mwa mgodi huo wapo mamia ya jamaa na marafiki wa wachimba migodi waliofukiwa ambao wanafuatilia kwa karibu shughuli za uokoaji.
Lakini mmoja wa wafanyakazi wa kikosi cha zimamoto amesema kuwa hamna matumaini makubwa ya kuwapata waliofukiwa wakiwa hai.
"Hakuna matumaini , kwani sidhani kuna uwezo wa mtu kusalia hai baada ya kufunikwa na matope haya kwa muda huu wote pasi na hewa "
Zima moto
Amesema serikali yake inapigana vita dhidi ya uovu huo.
Lakini mwandishi wa BBC ameongezea kuwa kuna migodi kadhaa katika maeneo yaliyojificha nchini humo.
Ijumaa wiki iliyopita, wachimba migodi wengine wanne walipoteza maisha yao huku sitini na watano wengine wakiathirika na gesi ya sumu katika sehemu ya Antioquia.
No comments:
Post a Comment