Ofisa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Bw. Suleiman Saleh akifuatilia kikao cha matayarisho ya maonesho hayo nchini humo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Vijimambo Bw. Baraka Daudi akitia saini kitabu cha wageni katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani siku kamati hiyo, ilipokutana na Ubalozi kwa kikao cha Maandalizi ya sherehe ya miaka 4 ya Vijimambo ambayo mwaka huu kauli mbiu yake ni kutangaza Utalii na kukemea ujangili kwa nguvu zote. Karibu tuungane pamoja katika siku hii maalumu ili wewe, mimi pamoja na yule wakiwemo watoto wetu wajifunze mengi kuhusu Utalii wa nchi yetu ukiwemo kukemea kwa nguvu zote suala zima la ujangili wa mali asili za nchi yetu.
Kaimu Katibu wa Kamati ya Vijimambo Bw. Julius Katanga akitia saini kitabu cha wageni kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani siku kamati ya maandalizi ilipokutana na Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kwa ajili ya maandalizi ya sherehe ya miaka 4 ya Vijimambo, itakayofanyika September 13, 2014.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akiongoza kikao, siku Kamati ya maandalizi ya sherehe ya miaka 4 ya Vijimambo ilipokutana na Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kwa ajili ya matayarisho ya mwanzo mwanzo ya sherehe hizo.
No comments:
Post a Comment