TANGAZO


Sunday, April 6, 2014

Waziri Mkuu Pinda aongoza mazishi ya Askofu Godfrey Mdimi, mjini Dodoma

*Awaonya watumishi wa Mungu kutojiingiza kusaka nafasi za uongozi kama wanavyofanya wanasiasa
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe, Mama Tunu Pinda, wakiweka mashada ya maua kwenye kaburi la Hayati, Askofu Godfrey Mdimi Mhogolo, wakati wa mazishi yake kwenye Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika jana. (Picha zote na John Banda, Dodoma)
Jenenza lenye mwili wa Hayati, Askofu Godfrey Mdimi Mhogolo, likiwa limeshawekwa kaburini kanisani hapo jana. 

Na John Banda, Dodoma
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amewambia Makasisi na watumishi wengine wa madhehebu ya dini Kutojiingiza kusaka nafasi za uongozi kwa njia kama wanazotumia wanasiasa kwani kwa kufanya hivyo wanamkaribisha shetani.

Pinda aliitoa rai hiyo jana, alipokuwa akitoa salamu za Serekali wakati wa ibada ya kuuombea mwili wa aliyekuwa Askofu wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Centrol Tanganyika, Godfrey Mdimi Mhogolo, iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu, aliyefariki mwishoni mwa mwezi uliopita alipokuwa kwenye matibabu nchini Afrika Kusini.

Waziri Mkuu alisema kuwa watumishi hao wa Mungu wapo tofauti na wanasiasa hivyo wanatakiwa kufuata utaratibu uliowekwa ndani ya madhehebu yao na si vinginevyo.

‘’Jamani sisi wenzenu tuliopo huko Serekalini huwa tunaamini kwenu ninyi wenzetu mnapokutana, kuna Roho Mtakatifu lakini sasa tukianza kusikia mambo kama haya maana yake mmemkaribisha shetani, siku nyingine inapoanza michakato kama hii unaweza kusikia nimeenda kwa wazee kule kijijini  kuwaomba msaada na isiwe ajabu’’, alisema pinda.

Awali Askofu Mkuu wa kanisa hilo Dk. Jacob Chimeledya alisema anashangazwa na baadhi ya Makasisi wa Dayosisi hiyo, kuanza kufanya kampeni za kuwania nafasi hiyo, iliyoachwa wazi na Mhogolo huku akiwaonya kuwa ni aibu kwa kanisa, mtu kuisaka nafasi hiyo mpaka kwa kutumia fedha.

Dk. Chimeledya aliyewafungia ndani ya kanisa hilo, makasisi wote mara baada ya mazishi na kuwaonya vikali kuhusu nia hiyo, Dayosisi hiyo, itakuwa chini yake mpaka hapo uchaguzi wa kumpata mwingine utakapofanyika.

Taarifa za ndani ya kikao hicho, kilichofanyika kwa saa 2 zilidai kuwa uchaguzi huo utafanyika mwishoni mwa mwaka huu.

No comments:

Post a Comment