TANGAZO


Tuesday, April 1, 2014

Vikao vya Kamati za Bunge Maalum la Katiba katika kujadili Sura ya Kwanza na ya Sita za Rasimu ya Katiba, zinazohusu Muungano, mjini Dodoma


* Wajumbe wataka siku ziongezwe kujadili Sura hizo

Mwenyekiti wa Kamati namba tano(5) ya Bunge Maalum la Katiba Hamad Rashid Mohamed (katikati) akiongoza mjadala wa Kamati hiyo leo mjini Dodoma wakati wanapitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya. (Picha zote na Bunge Maalum la Katiba (BMK), mjini Dodoma)
Mwenyekiti wa Kamati namba kumi na moja(11) Anna Kilango akiongea na waandishi wa habari juu ya mambo yaliyojitokeza katika kikao cha Kamati hiyo wakati wanapitia rasimu ya Katiba mpya. 
Mwenyekiti wa Kamati namba kumi na moja(11) Anna Kilango akiongea na waandishi wa habari juu ya mambo yaliyojitokeza katika kikao cha Kamati hiyo wakati walipokuwa wakitia rasimu ya Katiba mpya. 
Mwenyekiti wa Kamati namba kumi(10) ya Bunge Maalum la Katiba Paul Kimiti (katikati) akiongoza mjadala wa Kamati hiyo leo mjini Dodoma wakati wanapitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Machano Othman Said  akitoa mchango wake leo mjini Dodoma kuhusu muundo wa muungano unaofaa wakati wa kikao cha Kamati namba nne (4) kilichokuwa kinapitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya.

Wajumbe wa Kamati namba 10, wakiwa katika majadiliano kwenye kamati yao hiyo leo.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati namba nne (4) ya Bunge Maalum la Katiba, Dk. Sira Ubwa Maboya (kushoto), akiongoza mjadala wa Kamati hiyo leo mjini Dodoma wakati wanapitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa (kushoto), akijadiliana na Mjumbe mwenzake Selemani Jafo leo mjini Dodoma mara baada ya kikao cha asubuhi cha Kamati namba kumi (10) cha kupitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda (kulia) akitoa mchango wake leo mjini Dodoma wakati wa kikao cha Kamati namba mbili(2) kilichokuwa kinapitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya.
Mwenyekiti wa Kamati namba tatu (3) ya Bunge Maalum la Katiba Shamsi Vuai Nahodha  akiongoza mjadala wa Kamati hiyo leo mjini Dodoma wakati wanapitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya.
Baadhi ya wajumbe wa  Bunge Maalum la Katiba, Kamati namba nne (4) wakiwa katika kikao leo, mjini Dodoma cha kupitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba kwa ajili ya kuiboresha.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Salehe Nassoro Juma akitoa mchango wake leo mjini Dodoma kuhusu muundo wa muungano wakati wa kikao cha Kamati namba nne (4) kilichokuwa kinapitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Joseph Selethin akitoa mchango wake leo mjini Dodoma kuhusu muundo wa muungano unaofaa wakati wa kikao cha Kamati namba tano (5) kilichokuwa kinapitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda (kulia) akitoa mchango wake leo mjini Dodoma wakati wa kikao cha Kamati namba mbili(2) kilichokuwa kinapitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya.
 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda (kushoto) akitoa mchango wake leo mjini Dodoma wakati wa kikao cha Kamati namba mbili(2) kilichokuwa kinapitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya.
Mwenyekiti wa Kamati namba tano (5), Hamad Rashid Mohamed akiongea na waandishi wa habari juu ya mambo yaliyojitokeza katika kikao cha Kamati hiyo wakati wanapitia rasimu ya Katiba mpya.
Baadhi ya wajumbe wa  Bunge Maalum la Katiba, Kamati namba tano (5), wakiwa katika kikao leo, mjini Dodoma cha kupitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba kwa ajili ya kuiboresha.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa (kulia) akisamiliana na wajumbe wenzake leo mjini Dodoma mara baada ya kikao cha asubuhi cha Kamati namba kumi (10) cha kupitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Zendi Mvano Abdallah akitoa mchango wake leo, mjini Dodoma kuhusu muundo wa muungano unaofaa wakati wa kikao cha Kamati namba kumi (10), kilichokuwa kinapitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya.


Na Magreth Kinabo – Dodoma
KAMATI 12 za Bunge Maalum la Katiba, zimeaanza kazi vizuri ya kuchambua Rasimu ya Katiba, huku baadhi ya wenyeviti wakisema kuwa muda wa siku mbili wa kujadili sura ya kwanza na ya sita hautoshi.

 Hayo yamebainika  katika mahojiano  ya Mwenyekiti wa Kamati namba 11 ya Bunge hilo, Anne Kilango Malecela, yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa St. Gasper  mjini Dodoma leo.

“ Tatizo lililojitokeza ni kwamba muda wa siku mbili hautoshelezi, leo tumejadili sura ya kwanza sehemu ya kwanza kesho tutajadili sehemu ya  pili ya sura ya kwanza hivyo tunaweza tusiiguse sura ya sita.

“ Wenzetu walikataa Kanuni zisirekebishwe. Lakini  wenzetu wapinzani wameliona hilo wameanza kusema muda hautoshi,” alisema  Kilango.

 Aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo atamweleza Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samwel Sitaa (leo jioni ) kuwa  muda hautoshi.

Mwenyekiti huyo, alisema tatizo lingine lililojitokeza katika  kamati yake ni baadhi ya wajumbe kutokuwa na uelewa wa tofauti ya dola na nchi, hali iliyomfanya kutumia kanuni namba 56 (7) kumwomba Mwenyekiti wa Bunge hilo, ikiwezekana kumleta mtaalamu wa sheria ili kuweza kutoa elimu hiyo leo (jioni) juu ya masula hayo.

Akizungumzia kuhusu mjadala, alisema wajumbe wote walijitayarisha vizuri na walishindana kwa hoja hivyo hakuna aliyetoa maneneo makali.

Akizungumza kwa njia ya simu na waandishi wa habari nje ya ukumbi huo, kwa sababu alikuwa katika kikao, Mwenyekiti wa Kamati namba moja, Ummy Ali Mwalimu alisema  wajumbe walichangia kwa utulivu.

Ummy, alisema kilichojitokeza katika kamati yake ni kuwa muda hautoshi kama ilivyodaiwa na baadhi ya wajumbe kutoka upinzani, chama tawala na kutoka 201.

Naye  Mwenyekiti wa Kamati  namba tano (5) ya Bunge hilo, Hamad Rashid alisema kuwa katika kamati yake, mjadala uliendelea vizuri na ulikuwa wa kistaarabu.

No comments:

Post a Comment