Mkuu wa Mkoa wa Geita, Magalula Said Magalula akifungua
mkutano wa wadau mkoani Geita unatakaojadili mchakato wa uanzishaji wa Mfuko wa
Afya ya Jamii ujulikanao kama Tiba kwa Kadi (TIKA). (Picha zote na mpigapicha wetu)
Katibu Tawala wa Mkoa Severine Kahitwa akieleza umuhimu wa kuwa na utaratibu wa TIKA ndani ya Halmashauri ya Mji wa Geita.Wadau wa mkutano huo wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mkuu wa Mkoa huo.
Sehemu ya wadau wakisikiliza maagizo kutoka kwa mgeni rasmi ya namna ya kujadiliana katika mkutano huo.
Mkutano huo pia haukuwanyima fursa ya kuelewa
kinachozungumzwa ndani ya kikao hicho walemavu wa kusikia, mbele ni mkalimani
wa walemavu hao John Mukube.
Mkuu wa Mkoa Magalula Said Magalula akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya kundi maalum ambalo nalo limeshiriki mkutano huo.Wadau wakiwa makini kusikiliza mada zilizowasilishwa kwa ajili ya uanzishwaji wa TIKA mjini Geita.
Ofisa Masoko na Elimu kwa Umma kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Grace, akimshukuru mgeni rasmi kwa hotuba nzuri.
1. Wajumbe wakipitia mada zilizoandaliwa katika
mkutano huo.
1.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo wakiwa katika
picha ya pamoja.
Na
Mwandishi Wetu, Geita
MKUU
wa Mkoa wa Geita, Magalula Said Magalula, amezindua rasmi mchakato wa
uanzishwaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii ujulikanao kama Tiba kwa Kadi (TIKA), huku
akiwataka wadau kuhakikisha wanapitisha mpango huo kwa maslahi ya wananchi wa
mkoa huo.
Magalula
ameyasema hayo leo, wakati akizindua mpango huo kwa wadau mbalimbali kutoka
Halmashauri ya Mji wa Geita ambapo amesisitiza kuwa bila ya wananchi kujiunga
katika utaratibu wa TIKA itakuwa ni
vigumu kumudu gharama za matibabu ambazo zinaongezeka kila kukicha.
“Jamani
wenzetu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wametuletea mpango huu ni vyema
tukaujadili kwa makini na kwa mtazamo chanya ili hatimaye Halmashauri ya Mji
ianze utekelezaji wa suala hili…utaratibu wa kuchangia kabla ya kuugua ni mzuri
na unakupa uhakika wa kupata huduma za matibabu wakati wowote,” alisema Mkuu wa
Mkoa.
Alisema
kuwa wananchi wengi wamekuwa wakiingia kwenye matatizo mbalimbali yakiwemo ya madeni
ama kuuza vitu vya nyumbani kwa ajili ya kupata fedha za matibabu hali ambayo
imekuwa ikisababisha usumbufu mkubwa kwa familia husika hivyo akasisitiza
umuhimu wa kuanzishwa kwa TIKA ili kuondokana na matatizo hayo.
Hata
hivyo, Mkuu huyo wa Mkoa hakusita kuutaka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuhakikisha
unabadilika au kubadili mbinu zake za uhamasishaji kwa kuwafuata wananchi ambao
wako katika vikundi mbalimbali vya uzalishaji mbinu ambayo itarahisisha
kuwafikia wananchi wengi zaidi na uchangiaji wake utakuwa ni rahisi tofauti na
kumfuata mtu mmoja mmoja.
“Endeleeni
na uboreshaji wa huduma za matibabu na kuangalia ni namna gani mtamaliza au
kupunguza tatizo la ukosefu wa dawa katika vituo vya kutolea huduma ili
wananchi wasiwe na visingizio wakati wa kujiunga na mipango kama hii,” alisema.
Aidha
aliutaka uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Geita kuweka utaratibu mzuri wa
uwekaji wa kumbukumbu za wanachama kwa kuwa ndizo zinazotoa picha halisi ya
mahitaji yaliyopo ndani ya halmashauri ama mkoa kwa ujumla.
Akizungumzia
uboreshaji wa huduma za afya ndani ya Halmashauri hiyo, alimwagiza Mganga Mkuu
kutumia fursa zinazotolewa na NHIF za mikopo ya vifaa tiba na ukarabati wa
majengo kwa lengo la uboreshaji wa huduma za matibabu.
“Mbali
na fursa ya mikopo hii pia ni vyema matumizi ya fedha zitokanazo na CHF/TIKA i zikatumika kwa kufuata miongozo iliyotolewa
na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambayo asilimia 67 itumike kwa kununulia
dawa, asilimia 15 itumike kwa uboreshaji wa huduma za afya na inayobaki ndo
inaweza kutumika kwa shughuli zingine ambazo zinahusiana na masuala ya afya,”
alisema.
Kwa
upande wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ambao uliwakilishwa na Meneja wa CHF,
Constantine Makalla alisema kuwa lengo la Mfuko ni kuhakikisha kila halmashauri
inaanzisha na kutoa huduma kwa kuwa na sheria ndogo ambapo hadi Desema 31, 2013
jumla ya Halmashauri 128 zilikuwa na sheria ndogo.
Alisema
kuwa mipango ya NHIF kwa mwaka huu ni kuongeza uwigo wa wanachama, kuanza
utaratibu wa kuzizawadia Halmashauri zinazofanya vizuri na uboreshaji wa
daftari la CHF/TIKA na taarifa za wanachama wake nchi nzima.
No comments:
Post a Comment