TANGAZO


Friday, April 4, 2014

Rais wa Zanzibar Dk Ali Shein Atembelea Mnara wa Kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar Michezani na Uwanja wa mabembea wa Kariakoo Mjini Unguja

Uwanja wa mabembea wa Kariakoo Mjini Unguja ukiwa katika hatua za mwisho katika matengenezo, ambapo Rais wa wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, aliahidiwa kumalizika hivi karibuni wakati alipofanya ziara leo, ya kuona maendeleo ya ujenzi huo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akitembelea kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Mnara wa Kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar unaojengwa katika viwanja wa Kisonge Michenzani Mjini Unguja. (Picha zote na Ikulu Zanzibar)

No comments:

Post a Comment