Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, akisoma karatasi ya kupigia kura kabla ya kupia kura kumchagua Mbunge wa Jimbo la Chalinze kwenye kituo cha kupigia kura cha Zahanati ya Msoga, jimboni humo leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa kwenye chumba cha kupigia kura wakati wa kupiga kura za kumchagua Mbunge mpya wa Jimbo la Chalinze leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akipiga kura yake ya kumchagua Mbunge mpya wa Jimbo la Chalinze.
Mama Salma Kikwete, akiweka kura yake kwenye sanduku la kupigia kura kwenye kituo cha Zahanati ya Msoga leo.
Mgombea wa Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia Chama cha AFP, Ramadhani Mgaya akizungumza na waandishi wa habarai nje ya kituo cha Ofisi ya Mtendaji Kata namba 1 na kusema kuwa Chama chake kitakubali matokea yoyote na pia kama watashindwa watajipanga kwa ajili ya uchaguzi wa 2015.
Mgombea wa Ubunge Jimbo la Chalinze, Mathayo Torongey, akizungumza na baadhi ya mawakala alipotembelea kituo cha Ofisi ya Mtendaji, Kata namba 1, Bwilingu, jimboni humo leo.
Mgombea wa Ubunge Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Kikwete akihakiki taarifa zake kabla ya kupiga kura kwenye kituo cha Ofisi ya Mtendaji Kata namba 3 Bwilingu, Chalinze.
Aziza, mtoto wa mgombea wa Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia CCM, Ridhiwani Kikwete akimsaidia Baba yake kuweka kura kwenye sanduku la kura, Ridhiwani alipigia kura yake kwenye Kata ya Bwilingu.
Mkurugenzi wa Uchaguzi Jimbo la Chalinze, Samuel Salianga akizungumza na waandishi wa habari nje ya kituo cha Ofisi ya Mtendaji Kata ya Bwilingu na kutoa tathmini ya jinsi zoezi linavyoendelea na kufafanua mambo mbalimbali yanayohusu uhalali wa wagombea kupiga kura popote ndani ya jimbo la uchaguzi. (Na mpigapicha wetu)
No comments:
Post a Comment