TANGAZO


Friday, April 25, 2014

Nigeria yaahidi kuwatafuta wanafunzi


Wazazi wa wanafunzi walijaribu kwenda msituni wenyewe kuwatafuta watoto wao wakilaumu serikali kwa kujikokota
Juhudi za kuwaokoa zaidi ya wasichana 200 waliotekwa nyara na kundi la wanamgambo la Boko Haram, zimepewa kipaombele katika mkutano wa serikali kuhusu hali ya usalama nchini Nigeria.
Mkutano huo uliongozwa na Rais Goodluck Jonathan.
Wanaouhudhuria walikubaliana kuwa mgogoro kati ya wanajeshi wa serikali na kundi la wapiganaji wa kiisilamu Boko Haram, Kaskazini mwa nchi sio vita vya kidini bali vita dhidi ya raia wa Nigeria.Mkutano wenyewe uliodumu kwa saa sita, ulihudhuriwa na maafisa wakuu wa usalama , mawaziri na maafisa wakuu wa serikali kutoka pande zote..upande wa waisilamu na wakristo.
Juhudi za serikali kupambana na Boko Haram Nigeria zimeonekana kupatwa na changamoto nyingi
Wanafunzi zaidi ya miambili walitekwa nyara wiki jana na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram na kuwapeleka msituni.
Baadhi ya wasichana hao walifanikiwa kutoroka lakini wengine wengi wangali wanazuiliwa.
Wapiganaji hao wamesababisha vifo vya maelfu ya watu nchini humo wakidai kuwa wanapigania kile wanachosema ni misingi ya dini ya kiisilamu.
Kundi hilo pia lilikiri kufanya shambulizi baya katika kituo cha basi mjini Abuja wiki jana ambapo zaidi ya watu 70 waliuawa.

No comments:

Post a Comment