TANGAZO


Friday, April 4, 2014

Kikao cha mapendekezo ya marekebisho ya baadhi ya Kanuni za Bunge Maalum la Katiba, mjini Dodoma leo

Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samia Suluhu Hassan, akizungumza wakati alipokuwa akiendesha kikao cha kupitisha marekebisho ya Kanuni za bunge hilo, mjini Dodoma leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.BlogSpot.com)
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakisikiliza michango mbalimbali iliyokuwa ikitolewa na wajumbe wenzao kwenye bunge hilo leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, John Mnyika akichangia mapendekezo ya marekebisho ya Kanuni za bunge hilo, yaliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni, Pandu Ameir Kificho, bungeni humo leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mahamoud Thabit Kombo (kushoto), Mary Daffa (katikati) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. Mahadhi Juma Maalim, wakitafakari, wakati wa kujadili marekebisho ya Kanuni za bunge hilo leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba (kushoto) na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, mara baada ya kuaghirishwa kwa kikao cha bunge hilo leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba (kulia), akimueleza jambo mjumbe mwenzake, Dk. Mary Mwanjelwa, nje ya ukumbi wa Bunge, mara baada ya kuaghirishwa kwa kikao cha bunge hilo leo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Knuni ya Bunge Maalum la Katiba, Pandu Ameir Kificho akiwasilisha mapendekezo yamarekebisho ya kanuni, wakati wa kikao cha bunge hilo, mjini odoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba (kushoto), akimueleza jambo mjumbe mwenzake, Dk. Alshaima Kwagir, nje ya ukumbi wa Bunge, mara baada ya kuaghirishwa kwa kikao cha bunge hilo leo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Knuni ya Bunge Maalum la Katiba, Pandu Ameir Kificho, akimueleza jambo mjumbe mwenzake, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba (kushoto), nje ya ukumbi wa Bunge, mara baada ya kuaghirishwa kwa kikao cha bunge hilo leo.

Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Vicky Kamata (kushoto), Assumpter Mshama (katikati) na Dk. Mary Mwanjelwa, wakijadili jambo, nje ya ukumbi wa Bunge, mara baada ya kuaghirishwa kwa kikao cha bunge hilo leo.

Mwenyekiti wa Kamati namba 5 ya Bunge Maalum la Katiba, Hamad Rashid Mohamed, akizungumza na waandishi wa habari, mjini Dodoma leo, wakati alipokuwa akielezea kuhusu majadiliano kwenye kamati yake hiyo, aliyosema wamemaliza majadiliano ya Sura ya Kwanza na ya Sita ya Rasimu ya Pili ya Katiba ambapo wajumbe wengi wamependekeza Muungano wa Serikali mbili wenye marekebisho mbalimbali. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wake, Assumpter Mshama.
Mwenyekiti wa Kamati namba 6 ya Bunge Maalum la Katiba, Stephen Wasira, akizungumza na waandishi wa habari, mjini Dodoma leo, wakati alipokuwa akielezea uhusu majadiliano kwenye kamati yake hiyo na hatua iliyofikiwa ambapo alisema wajumbe wengi katika kamati hiyo kwa sura za Kwanza na Sita walikuwa wakipendekeza Muungano wa Serikali mbili wenye marekebisho mbalimbali.

No comments:

Post a Comment