TANGAZO


Wednesday, April 2, 2014

Kamati ya Kuzuia mauaji ya Kimbari na uhalifu wa kivita yaelezea mikakati ya kulinda amani, kuzuia uhalifu na kupiga ubaguzi nchini

Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari na Uhalifu wa Kivita Bi Felistus Joseph (wa kwanza kushoto), akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo, kuhusu mikakati ya Kamati hiyo katika kulinda amani, kuzuia uhalifu na kupinga ubaguzi hapa Nchini. Katikati ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bi Farida Khalfan na mwisho ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Bi Fatma Salum.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bi Farida Khalfan akiwaeleza waandishi wa Habari (hawapo pichani) nafasi ya vyombo vya Habari katika kuzuia mauaji ya Kimbari. Kushoto ni  Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari na Uhalifu wa Kivita Bi Felistus Joseph.
Waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia mkutano wa Kamati ya Kitaifa ya kuzuia Mauaji ya Kimbari na Uhalifu wa Kivita. (Picha zote na Georgina Misama-MAELEZO) 

No comments:

Post a Comment