TANGAZO


Wednesday, April 2, 2014

Maadhimisho ya Kimataifa ya kumbukumbu ya miaka 20 ya mauaji ya kimbari kuadhimishwa nchini

*Balozi wa Rwanda nchini Tanzania azungumza na waandishi wa habari

Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Dk. Benjamin Rugangazi, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu maadhimisho ya miaka 20 ya kumbukumbu ya mauaji ya kibari, yaliyotokea nchini humo, mwaka 1994. Maadhimisho hayo yatafanyika Aprili 7 na mgeni rasmi atakuwa ni Waziri katika Ofisi ya Rais, asiye na Wizara Maalum, Profesa Mark Mwandosya.
Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Dk. Benjamin Rugangazi, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu maadhimisho hayo ya miaka 20 ya kumbukumbu ya mauaji ya kibari, yatakayofanyika jijini Dar es Salaam April 7. Kulia ni Ofisa Habari Kituo cha Kimataifa (UNIC), Stella Vuzo.
Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Dk. Benjamin Rugangazi, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo,, kuhusu maadhimisho hayo ya miaka 20 ya kumbukumbu ya mauaji ya kibari, yatakayofanyika jijini Dar es Salaam April 7. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Maelezo, Assah Mwambene.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Maelezo, Assah Mwambene, akimweleza jambo Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Dk. Benjamin Rugangazi (kulia), wakati alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari, yatakayofanyika Aprili 7 jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari, wakisikiliza maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Dk. Benjamin Rugangazi, wakati alipozungumza nao Dar es Salaam leo,kuhusu maadhimisho ya miaka 20 ya kumbukumbu ya mauaji ya kibari, yatakayofanyika jijini Dar es Salaam April 7. (Picha zote na Maelezo)

No comments:

Post a Comment