Mkufunzi mkuu na meneja wa klabu ya Manchester United David Moyes ametimuliwa.
David Moyes amefutwa kazi baada ya kushikilia usukuni wa klabu hiyo kwa miezi kumi tu.Klabu hiyo hapo awali ilikuwa imekataa kuzungumzia udaku wa magezti kuwa Moyes atafutwa kazi kabla ya msimu kumalizika.
Moyes, mwenye umri wa miaka 50, aliteuliwa na Ferguson kumrithi alipostaafu mwaka jana baada ya kuwa na klabu hiyo kwa miaka 26.
Taarifa kutoka kwa klabu hiyo imemshukuru Moyes kwa bidii, uaminifu na hekima aliyoonyesha kocha huyo akiwa mkufunzi wa Manchester United.
Moyes alichukuwa usukani wa kuifunza Manchester United mwaka uliopita baada ya aliyekuwa kocha wa siku nyingi Sir. Alex Ferguson kustaafu.
Huku zikiwa zimesalia mechi nne pekee msimu wa ligi kukamilika Mancheseter united inashikilia nafasi ya saba kwenye jedwali la msimamo wa ligi hiyo alama ishirini na tatu nyuma ya viongozi Liverpool.
Klabu hiyo imeshindwa kufuzu kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa ulaya kwa mara ya kwanza katika kipindi cha takriban miaka ishirini.
No comments:
Post a Comment